MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam, imemwacha huru Raia wa Kenya, Joshua Muhindi
(22) aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumteka na kujaribu kumwua
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka.
Hata hivyo, baada ya kuachwa jana, muda mfupi baadaye alikamatwa tena na kusomewa mashitaka ya kutoa taarifa za uongo kwa Ofisa wa Jeshi la Polisi.
Muhindi aliachwa na Hakimu Waliarwande Lema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwasilisha hati ya kufuta kesi hiyo kwa kuwa hana haja ya kuendelea nayo.
Alikamatwa tena, na saa 6.15 mchana akapandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana na kusomewa mashitaka mapya.
Katika mahitaka hayo mapya, Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa Julai 3 mwaka jana katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, Muhindi alitoa taarifa za uongo Polisi, kuwa yeye na wenzake ambao hawajulikani, walikodishwa kumteka na kumwua Dk Ulimboka jambo ambalo si kweli.
Mshitakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo

umekamilika na kuomba tarehe ya kutajwa kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.
Muhindi aliiomba Mahakama impe dhamana, kwa kuwa ana wadhamini, hata hivyo upande wa mashitaka ulipinga ombi hilo ukidai ni kutokana na usalama wake kwa kwa kuzingatia mazingira ya kesi hiyo na maslahi ya umma.
Aidha, Wakili Kweka alidai kuwa mshitakiwa si raia wa Tanzania pia hana makazi maalumu hivyo itakuwa vigumu kumpata. Hata hivyo, Muhindi alidai kuwa ameshakaa rumande tangu mwaka jana na kitendo cha kumrudisha gerezani ni kujaribu kumpoteza ili kutuliza umma na Bunge na kudai endapo atarudi gerezani, atagoma kula na ataandamana.
"Hawa watu wanataka kunipoteza mimi kijana mdogo wa miaka 22 na mashitaka yanayonikabili si ya kweli, naumia sana Mheshimiwa" alidai Muhindi mbele ya Hakimu.
Hakimu Katemana alisema kama upande wa mashitaka unataka kupinga dhamana uwasilishe hati mahakamani kabla ya saa 7.30 mchana jana, lakini ulishindwa kufanya hivyo.
Muhindi aliachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili, mmoja akifanya kazi katika taasisi inayojulikana ambapo walisaini hati ya Sh milioni tano na yeye kusaini ya Sh milioni tano na kuwasilisha pasipoti yake.
Kesi itatajwa Agosti 20. Mara ya kwanza Muhindi alifikishwa mahakamani hapo Julai 13, mwaka jana akidaiwa kuwa Juni 26 mwaka huo, katika eneo la Leaders Club, alimteka Dk Ulimboka.
Katika mashitaka mengine, ilidaiwa kuwa siku hiyo hiyo, akiwa eneo la Msitu wa Mabwepande, Dar es Salaam, kinyume cha sheria alijaribu kumsababishia kifo Dk Ulimboka, alikana mashitaka hayo.
Rejea: HabariLeo

0 comments:
Post a Comment