Tuesday, 27 August 2013

CHUO KIKUU CHAWEKA UTARATIBU WA KUVAA KOFIA ILI KUZUIA WANAFUNZI KUIBIA MAJIBU

Wakufunzi katika chuo kimoja huko nchini Thailand wamelazimika kufuta utaratibu wa wanachuo kuvaa kofia zilizoundwa kwa makaratasi katika vyumba vya mitihani ili kuzuia wasichunguliane mitihani na majibu.

Picha mbili zilizowekwa kwenye ukurasa wa Facebook (sasa hivi zimeondolewa), zilionesha namna wanafunzi hao walivyokuwa katika moja ya vyumba vya mtihani. Watu waliotoa maoni mbalimbali walipinga vikali na hata kulaani uvaaji kofia hizo.

Mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho aliyehojiwa na chombo kimoja cha habari kuhusu utaratibu huo, alisema kuwa ni mbinu waliyokuja nayo wanachuo wenyewe walipoulizwa ni kwa namna gani wanadhani wanaweza kujilinda wenyewe dhidi ya kuibia majibu ya mitihani, na asiliani haukuwa utaratibu wa chuo. Mhadhiri huyo akasema kwa kuwa picha hizo zimeibua gumzo na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wahadhiri wa chuo  hicho, wamelazimika kufuta utaratibu huo na kuwaomba wanachuo watunge mbinu mpya.

Baadhi ya wachuo walihuzunika kwa mbinu yao kupokelewa vibaya, tofauti na walivyoifurahia wao.
Picture
Hii nipicha ya wanafunzi wa Kasetsart University wakifanya mtihani  (picha na: odditycentral.com)

Picture 
habari kwa hisania ya The NPR.

 

0 comments: