Kiungo wa
Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’ ameonyesha kuridhishwa na hali ya kujituma kwa
wachezaji wenzake wa timu hiyo, lakini akawashushia onyo kali kabla ya kuanza
kwa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013/2014, unaoanza kesho Jumamosi.
Yanga itafungua
pazia la ligi hiyo kesho kwa kukipiga dhidi ya Ashanti kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
Chuji alisema hana mashaka juu ya uwezo wa kikosi hicho,
lakini amewataka nyota wenzake wa timu hiyo kuwa makini katika michezo yao kwa
kuwa kila mechi watakayocheza ni kama fainali.
“Najua jinsi
gani tunavyokuwa tunakamiwa katika ligi, hii imekuwa ikijitokeza katika kila
mchezo, sasa ni lazima mimi na wenzangu tujiandae kwa hali hiyo, tuna timu
nzuri lakini kama hatutaonyesha juhudi itakuwa ni kazi bure,” alisema Chuji.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment