TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe
unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa
asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.
Mkoa wa
Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma
(7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9),
Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mikoa
mingine na viwango vyake ni Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10),
Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida
(3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja
(1.9) na Pemba (0.3).
Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti
uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo,
alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema
watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya
ukimwi na UKIMWI wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo
mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume endapo
inapunguza maambukizi ya UKIMWI alisema inapunguza kwa asilimia 60 na
kusisitiza kuwa ipo haja kutoa elimu zaidi juuya uelewa wa ugonjwa huo.
---via Habari Leo
Tuesday, 6 August 2013
HOME »
» MKOA WA NJOMBE WAONGOZA KWA MAMBUKIZI YA UKIMWI TAKWIMU ZA TACAIDS ZA ONYESHA
0 comments:
Post a Comment