Hawa ni wafanya biashara wa masoko ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwa katika kikao
Na Nathan Mtega,Songea
UMOJA wa
wafanyabiashara wa masoko ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umeendelea
kuulalamikia uongozi wa Manispaa ya Songea kwa kuongeza gharama za pango la
vibanda na gharama za leseni za biashara kwa wafanyabiashra pamoja na utaratibu
usioridhisha wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hali hiyo imepelekea
wafanyabiashara hao kuazimia kugoma.
Wakizungumza katika mkutano wa dharula wanachama zaidi ya themanini
wa umoja huo wamesema hawakubaliani na utaratibu wa uendeshaji wa masoko
yaliyopo ndani ya manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na ogezeko la pango
lililoamriwa na uongozi wa manispaa bila kuwashirikisha wafanyabiashara hao.
Wamesema uwezo wa wafanyabiashara katika masoko ya Manispaa
ya songea na mzunguko wa fedha uliopo hauendani na ongezeko hilo la kodi,ushuru
na utaratibu wa kuwataka wafanyabiashara hao
kuomba tenda ya kuendelea kufanya biashara katika vibanda hivyo
walivyokuwa wakifanyia biashara zao.
Wakizungumza wafanyabiashara Christian Kayombo na Hamis Machaku
katika mkutano huo wamesema kuwa utaratibu unaofanywa na uongozi wa Manispaa wa
kuongeza pango la vibanda na kutangaza tenda kwa ajili ya vibanda hivyo ambavyo
wao wamekuwa wakivitumia kwa mkataba wa muda mrefu bila kushirikishwa kwenye maamuzi hayo
mapya ni ishara ya unyanyasaji kwao na hawajatendewa haki kwa sababu
walishaomba kupunguzwa kwa kodi pamoja na malipo ya leseni lakini kabla maombi
hayo hayajafanyiwa kazi wanaletewa ongezeko la kodi.
Wamesema kuwa ni
vyema uongozi wa Manispaa ukaona umuhimu wa kuwashirikisha wafanyabiashara kwa
kupitia viongozi wa umoja wao katika kutoa na kufikia maamuzi yanayowahusu
badala ya uongozi huo kukaa na kuamua juu ya wafanyabiashara wakati ukijua hali
za biashara katika Manispaa ya Songea na mzunguko wa fedha ulivyo.
Aidha wafanyabiashara hao wametangaza kugoma siku ya Jumanne 6 Agosti 2013 kwa muda
usiojulikana kuendesha biashara ikiwa malalamiko hayo hayatafanyiwa kazi kwa
sababu kumekuwepo na vitendo vingi vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya
watumishi wa halmashauri dhidi ya wafanyabiashara na hususani wafanyabiashara
wadogo .
Akizungumza makamu mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa
masoko ya Manispaa ya Songea Leornad Chiwangu alisema wafanyabiashara
wameazimia kuanza mgomo huo siku ya Jumanne na utaendelea kwa muda usiojulikana
ikiwa malalamiko na maombi yao hayatafanyiwa kazi.
Na Nathan Mtega,Songea
0 comments:
Post a Comment