Wednesday, 21 August 2013

AFIKISWA KOTINI KWA HEROINI NA BANG MAHAKAMA YA MAKAZI KISUTU


MFANYABIASHARA Edson Monyo (39), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na makosa mawili ya kukutwa na dawa za kulevya zenye thamani ya sh milioni 68.

Wakili wa Serikali, Leonard Chalo, mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alidai mshitakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili, ambapo Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere alikamatwa akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya sh 68,069,250.

Wakili Chalo alidai kosa la pili alilitenda tarehe na eneo hilo hilo ambalo ni kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 34.77 yenye thamani ya sh 13,908, na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hata hivyo Hakimu Riwa alimtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote katika shitaka la kwanza kwa sababu mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza kosa hilo na akamtaka ajibu katika kosa la pili na mshitakiwa huyo alikanusha kutenda kosa hilo, hakimu huyo aliamuru mshitakiwa huyo arejeshwe rumande hadi Septemba 3, mwaka huu, kesi yake itakapokuja kwa ajili ya kutajwa


na Happiness Katabazi


.

0 comments: