TAMASHA la ziara za washindi wa Tuzo za Kilimanjaro ‘Kili Music Tour
2013’, linaloandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake
ya Kilimanjaro, linatarajiwa kufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa New
City Pub, mkoani Mbeya.
Wiki iliyopita, tamasha hilo lilifanyika jijini Mwanza, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya walipamba tamasha hilo.
Akizungumza jana, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, alisema tamasha hilo litakuwa la aina yake, baada ya lile lililofanyika jijini Mwanza.
Aliwataja wasanii watakaopamba tamasha hilo mkoani Mbeya kuwa ni Linex, Fid Q, Barnaba, Prof Jay, Kala Jeremiah, Ben Paul, Izzo Bizness, Snura na Awilo wa Mbeya.
“Tunashukuru kuwa Watanzania wamepokea tamasha hili kwa moyo mkunjufu kabisa na walishiriki kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Mwanza,” alisema Kavishe.
Chanzo gazeti la mtanzania
Alhamisi, Agosti 22, 2013 06:20
Na Gilbert Massawe, Dar es Salaam

0 comments:
Post a Comment