HOME »
» TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU SHEIKHE ALIYE CHOMWA KISU AKIENDESHA IBADA YA IDD MKOANI MBEYA
|
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani |
|
Msikiti wa Ijumaa wa mjini Kyela ambao Shekhe wa msikiti huo alivamiwa na kupigwa wakati wa swala ya Idd leo asubuhi |
TAARIFA YA JESHI LA POLISI
WILAYA YA KYELA - WATUHUMIWA SITA WADHIBITIWA NA WAUMINI KWA USHIRIKIANO NA MAKACHERO WA POLISI WALIPOTAKA KUANZISHA FUJO.
MNAMO
TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO ENEO LA BONDENI KATIKA
MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. NURU S/O
MWAFILANGO,MIAKA 77,KYUSA,SHEKHE MKUU WA WILAYA YA KYELA, MKAZI WA
BONDENI AKIWA ANAONGOZA IBADA YA SWALA YA IDD EL FITRI MSIKITINI HAPO
ALIVAMIWA NA BAADHI YA WAUMINI WANAOJIITA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI
NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUTUMIA FIMBO,NONDO,MKASI NGUMI NA MATEKE
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. CHANZO NI
MADAI KUWA HAWAMTAKI SHEKHE HUYO KWA MADAI KUWA HANA UWEZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA WAKATI
WAUMINI WOTE WAKIWA WAMEINAMA WAKISWALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA. MHANGA
HAKUPATA MADHARA BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKIANA NA
POLISI/MAKACHERO WA-KIISLAMU KUMUOKOA. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA
SITA AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1.MASHAKA
S/O KHASIMU,MIAKA 30,MUHA,MKULIMA MKAZI WA NDANDALO 2. ISSA S/O JUMA,
MIAKA 37, MRANGI, MKULIMA,MKAZI WA BONDENI 3.AHMED S/O KHASIMU @
MAGOGO,MIAKA 35,MPOGORO,MKULIMA/MGANGA WA KIENYEJI, MKAZI WA MBUGANI
[ALIKUTWA NA MKASI] 4. IBRAHIM S/O SHABAN,MIAKA 17,KYUSA,MWANAFUNZI
SHULE YA SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA NNE MKAZI WA NDANDALO [ALIKUTWA
NA FIMBO KUBWA NA NDIYE ALIYEMNYANG’ANYA SHEKHE KIPAZA SAUTI] 5.
AMBOKILE S/O MWANGOSI @ ALLY,MIAKA 19,KYUSA,MWANAFUNZI WA SHULE
YA SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA TATU, MKAZI WA BONDENI [ALIKUTWA NA
KIPANDE CHA NONDO] NA 6. SADICK S/O ABDUL, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA,
MKAZI WA NDANDALO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KATIKA
TUKIO HILO HAMIS S/O HUSSEIN, MIAKA 50, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA BONDENI ALIPATA MAJERAHA KIDOGOKWA KUKATWA MKASI JUU
YA SIKIO LA KUSHOTO WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMUOKOA MHANGA
ASIPATE MADHARA NA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HALI YA USALAMA
NA AMANI ILIREJEA MUDA MFUPI NA WAUMINI WALIENDELEA NA IBADA YAO
CHINI YA UONGOZI WA SHEKHE HUYO NA KUMALIZA SALAMA. HAKUNA UHARIBIFU WA
MALI ULIOTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAUMINI NA JAMII KWA UJUMLA
KUTATUA MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA KUKAA KWENYE MEZA
YA MAZUNGUMZO BAADA YA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANASISITIZA KUWA KWA
YEYOTE ATAKAYEJARIBU /ATAKAYEVUNJA SHERIA HATAFUMBIWA MACHO.
Imesainiwa na,
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Mbeya
— WAUMINI wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika ibada ya Swala ya Idd El
Fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo Wilayani Kyela mkoani Mbeya
wamekumbwa na taharuki baada ya Shekhe wao aliyekuwa akiongoza ibada
kuvamiwa kibla wakati akiendesha ibada na kujeruhiwa.
Tukio hilo
la aina yake limetokea majira ya asubuhi ambapo Shekhe huyo
aliyetambuliwa kwa jina la Nuhu Mwafilango alishambuliwa akiwa katikati
ya sijida baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa shule ya
sekondari ya kutwa ya Kyela, Ally Mwangosi kuchoma Shekhe huyo na kitu
chenye ncha kali.
Taarifa kutoka msikitini hapo zinadai kuwa mara
baada ya tukio hilo, Shekhe alipiga kelele wa kuomba msaada na ndipo
waumini waliokuwa wakiswali msikitini hapo waliposhikwa na taharuki.
Mwenyekiti
wa Baraza Kuu la Waislamu Wilayani Kyela Bw. Daudi Mwenda alisema kuwa
waumini walimuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Bw. Mwenda alisema kuwa Shekhe huyo ameumizwa
vibaya kichwani na kutokwa na damu nyingi. Waumini wawili waliojaribu
kumuokoa Shekhe huyo nao walijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu ikiwa ni
pamoja na mweka hazina wa BAKWATA wilaya Ustadhi Khamis Hussein ambaye
alijeruhiwa kichwani na sikioni.
Nao baadhi ya waumini
waliokuwepo katika ibada hiyo walisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati
waumini wote wakiwa wamesujudu, ndipo waliposikia kelele na vurugu.
Mmoja
wa waumini aliyejitambulisha kwa jina la Idd Hussein alisema kuwa
liliibuka kundi la watu waliomsaidia kijana huyo, na kuibua vurugu kubwa
iliyosababisha ibada ya swala ya Idd kuvunjika.
Akizungumzia
tukio hilo Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Shekhe Juma Killah alisema
kuwa vurugu hizo zimetokea katika swala ya Idd na wahusika wa vurugu
hizo ni Waislamu ambao... Read more
0 comments:
Post a Comment