Thursday, 15 August 2013

RIPOTI MAALUMU: ELIMU BUKOMBE MAJANGAA

 

 

Wanafunzi wa moja ya shule zilizopo katika Wilayani Bukombe, kama walivyokutwa na mpigapicha wetu 
Na Neville Meena na Jacqueline Masinde, Mwananchi   
0
Share
Bukombe:
Wakati Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikizindua Mpango wa Kuleta Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika Sekta ya Elimu Tanzania leo, maelfu ya watoto wenye umri wa kwenda shule katika vitongoji kadhaa vya Kijiji cha Namalandula, mkoani Geita wanasoma katika mazingira duni kutokana na shule walizozianzisha kutosajiliwa hadi sasa.Waziri wa Elimu, Dk Shukuru Kawambwa ndiye atakayezindua mpango huo leo sambamba na maonyesho yenye lengo la kuelimisha na kupata maoni ya wadau katika utekelezaji wa vipaumbele vya sekta ya elimu.



Wakati hayo yakiedelea, katika vitongoji vya Ilyamchele na Mutukula vilivyopo Wilaya ya Bukombe zimejengwa shule za msingi ambazo kwa muda wote wa uhai wake unaokaribia miaka 10, zimekuwa zikitoa ‘elimu ya awali’ tu, licha ya kwamba zina madarasa kadhaa.Maisha ya kielimu katika shule hizi ni ya kuhuzunisha kutokana na kwamba hazijasajiliwa hali ambayo ina athari kubwa kwa maelfu ya watoto wanaosoma hapo sasa na wale ambao wamewahi kusoma hapo.Mazingira ya shule zote mbili ni duni na hazina miundombinu kwani madarasa 

yamejengwa kwa miti na baadhi yake yameezekwa kwa nyasi. Idadi kubwa ya watoto inawafanya walimu wa kujitolea katika shule hizi kuchanganya madarasa.Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Namalandula, Jackson Bwire anasema shule hizo zilianzishwa na wananchi kutokana na kutokuwapo kwa huduma za elimu katika maeneo yao ambayo yana kaya zaidi ya 3,500 hivi sasa, zenye watoto wapatao 7,000 na kwamba nusu yao wanapaswa kuwapo shuleni wakisoma.

Mwananchi lilishuhudia katika Shule ya Ilyamchele wanafunzi wakisoma kwa zamu (wengine asubuhi na wengine mchana) wakati katika Shule ya Mutukula, darasa la kwanza wanasoma peke yao kutokana na wingi wao wakati darasa la pili wanachangamana na la tatu na darasa la nne wanachanganyika na darasa la tano.Awali wanafunzi katika shule hizo walikuwa wakisoma mpaka ‘darasa la sita’ lakini sasa wengi wanaishia darasa la nne,

 kisha kupelekwa katika Shule ya Msingi ya Namalandula ambako hufanya mtihani wa darasa la nne na wenzao kwa lengo la kuendelea na darasa la tano baadaye.Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Namalandula, Jackson Bwire aliliambia gazeti kuwa baadhi ya watoto ambao walifaulu darasa nne wameshindwa kuendelea darasa la tano kutokana na umbali uliopo kutoka katika vitongoji wanakotoka na ilipo shule iliyosajiliwa. 

Wingi wa wanafunzi 
Hivi sasa shule hizi kwa pamoja zina wanafunzi 954; Ilyamchele ambayo pia inajulikana kama Kashishi ikiwa na wanafunzi 600 na walimu watatu wakati shule ya Mutukula ina wanafunzi 354 na walimu watano.Mwezi Mei mwaka huu Shule ya Ilyamchele ambayo ilianzishwa mwaka 2004 ilikuwa na na wanafunzi 783; wavulana 402 na wasichana 381 wakati Shule ya Mutukula ambayo ilianzishwa 2008, ilikuwa na wanafunzi 410; wavulana 183 na wasichana 327

0 comments: