Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa
Ponda akiwa na wakili wake, Juma Nassoro katika Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (Moi), jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
Baraza Kuu la Waislam
Tanzania, BAKWATA, limeitaka serikali kuunda tume huru ya uchunguzi na
kumtaka kamanda wa polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile kujiuzulu
ili kupisha tume hiyo itakayoundwa kulifanyia uchunguzi tukio la katibu
wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda kupigwa
risasi na polisi mkoani humo huku familia yake ikitoa msimamo wao
kuhusiana na tukio hilo.
ILANI: Nakala ya maansishi ifuatayo inayoelezea hali ya marejra ya Sheikh Ponda imepatikana mtandaoni, MBEYAGREENNEWS.BLOGSPORT.COM
haina uthibitisho kama imetolewa na MOI kama inavyosomeka, ikithibitika sivyo, itaondolewa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAJERAHA YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA
Dar es salaam 12/8/2013
Sheikh Ponda Issa Ponda (54) alipokelewa hapa taasisi ya ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 jioni akitokea hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe
kipimo cha X-ray ili ubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha tathimini ya madaktari baada ya kupata majibu ya X-ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo.
KWA HIYO
1- kufwatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla kabla ya kufikishwa moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani
2- kipimo cha X-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana
3- hivyo basi Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea n matibabu baada ya upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu MOI
0 comments:
Post a Comment