Saturday, 31 August 2013

TAZARA YAHAIRISHA KUFUKUZA WAFANYAKAZI YASEMA WAREJEE KAZINI ITAWARIPA MISHAHARA YAO

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imesitisha kusudio lililotangazwa awali, la kufukuza wafanyakazi wake wapatao 1,067 na kuagiza warudi kazini kuanzia leo.

Kaimu Mkurugenzi wa TAZARA, Ronald Phiri, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari. Aliongeza kuwa mbali na kurudishwa kazini, mishahara yao itaanza kulipwa leo.

“Kwa kuwa hakuna aliyepewa barua ya kusimamishwa kazi mpaka sasa hivi, basi ni halali kusema kuwa hakuna aliyefukuzwa kazi TAZARA. Mazungumzo bado yanaendelea na wafanyakazi wote wanaombwa kurudi kazini kwa sababu tayari tuna fedha na tutaanza kuwalipa mishahara yao kesho (leo),” alisema Phiri.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alionya kuwa ambaye hataripoti kazini leo, atakuwa amejisimamisha kazi mwenyewe na hatohesabika tena kama mfanyakazi wa TAZARA. (kwa hisani ya HabariLeo)

TAZARA imekubali kuwalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wake baada ya kuendesha mgomo wa siku saba. Uamuzi huo umefikiwa baada ya TAZARA kukaa na uongozi wa wafanyakazi hao. (kwa hisani yaMWANANCHI)


 

0 comments: