Sunday, 18 August 2013

DR REGINALD MENGI ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA TPSF

 

 
 Mkutano mkuu wa 14 wa Taasisi ya sekta binafsi  nchini (TPSF)umemchagua  Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi kuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na Bw. Salum Shamte kuwa makamu wake.
 
Msimamizi wa uchaguzi huo katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara  Bi. Joyce Mapunjo ametangaza matokeo hayo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu  huo  ambao pia ulichagua wajumbe  kumi na moja wa  bodi mpya ya taasisi ya sekta binafsi nchini  baada ya bodi iliyokuwepo ikiongozwa na Bi. Esther Mkwizu kumaliza muda wake.

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa mwenyekti mpya wa TPSF Dr. Reginald Mengi  amesema bodi yake itaendelea  kushirikiana na serikali  katika  kujenga uchumi  imara kwa watanzania huku akisisitiza  suala la ardhi  liangaliwe kwa mtazamao mpana zaidi.

Kwa upande wake  mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi nchini  bw. Godfrey Simbeye  amesema bado taasisi hiyo  ni changa  na ana matumaini  bodi hiyo itafanya yale yatakayoipeleka  nchi katika uchumi imara zaidi.

Wajumbe wapaya wa bodi ya taasisi ya sekta binafsi  ni  Dr. Reginald Mengi, Salum Shamte, Felix Mosha, Dr. Gideon Kaunda, Dr. Charles kimei ,Deo Mwanyika,Enock Ndondole, Mbarouk omar  mohamed, Anna Matinde, Gaudence Temu na  mhandisi  Peter Chisawilo.

0 comments: