Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage yuko mjini Bujumbura kufanya juhudi za kupata ITC za
wachezaji wawili, Kaze Patrick ‘Demunga’ na Amis Tabwe.
Wachezaji hao
walishindwa kucheza mechi ya jana wakati Simba ilipoivaa Rhino ya Tabora na
kutoka sare ya mabao 2-2.
Kutokana na
hali hiyo, Rage amefunga safari hadi Burundi ili kuhakikisha suala hilo
linafanikiwa.
“Kweli Rage
yuko Bujumbura kupambana na hili suala, kidogo Warundi wanataka kutufanyia kitu
ambacho si sahihi. Wanasema wana mikataba na hao wachezaji, lakini hawataki
kuionyesha kwa kuwa wachezaji wenyewe wanasema hawana mikataba na Vital’O,”
alisema mpasha habari.
Awali imeelezwa
kuwa, Shirikisho la Soka la Burundi linataka kufanya njama ili kuhakikisha
wanabaki kuwa wachezaji wa Vital’O ili liwatumie katika michuano ya Chan nchini
Afrika Kusini kwa kuwa Burundi imefuzu.
Burundi ilifuzu
katika michuano hiyo kwa kuwatoa Sudan na wachezaji hao walikuwa sehemu ya
chachu ya ushindi huo.
Chanzo salehjembe blog
0 comments:
Post a Comment