Ushauri
umetolewa na Meneja Uhusiano wa Super Market ya TSN, Meshack Nzowah,
wakati wa promosheni ya kinywaji cha Chilly
Willy iliyofanyika jijini
Dar es Salaam ambapo amewataka watu wenye matatizo na maradhi ya moyo
kutotumia kinywaji hicho ili kujiepusha na matatizo ambayo yanaweza
kuwapata kama wanatumia kinywaji hicho pasipo kujua madhara yake.
Watu wengine ambao hawatakiwi kutumia kinywaji hicho ni watoto walio chini ya miaka 10.
Akizungumza katika hafla hiyo Nzowah alisema Chilly Willy ni kinywaji kisicho na kilevi kinatumika kwa watu mbalimbali na kinaongeza nguvu kwa watumiaji, lakini kwa watu wenye matatizo ya moyo hakiwafai.
Aliongeza kuwa kinywaji hicho kinachotengenezwa Dubai, kinapendwa na watu mbalimbali duniani hususan wanamichezo na kimekuwa kikiwaongezea nguvu.
“Baada ya kuona kinywaji cha Chilly Willy kinatumiwa na watu wengi duniani, tumeamua kukileta Tanzania ili watu waanze kukitumia kwa kweli ni kinywaji bora na kinakata uchovu wa pombe,”alisema Nzowah. ---

source MAJIRA
0 comments:
Post a Comment