Monday, 26 August 2013

MATAPELI WAKIMATAIFA WAJIPENYEZA SERIKANI NA WAWEKEZAJI WA KIGENI WALIZWA MAMILION

*Matapeli wa kimataifa wajipenyeza serikalini
*Wawekezaji wa kigeni walizwa mamilioni

MTANDAO wa matapeli wa kimataifa ambao umekuwa ukiendesha shughuli zake haramu sehemu mbalimbali duniani, sasa umejipenyeza katika taasisi na vyombo vya dola hapa nchini, MTANZANIA Jumatatu linaripoti.

Kubainika kwa mtandao huo hapa nchini, kumetokana na kuvuja kwa taarifa za siri za baadhi ya wawekezaji wa kigeni ambao wametapeliwa mamilioni ya Dola za Marekani na watu ambao wamekuwa wakijitambulisha kwao kuwa ni maofisa wa Serikali au makamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wenye ushawishi serikalini.

Vyanzo vya habari vya MTANZANIA Jumatatu vilivyoko serikalini vimedokeza kuwa, wawekezaji waliokutana na dhahama hiyo ni wale ambao wanajihusisha na biashara ya madini kwa kificho mbali na kuendesha shughuli zao halali zinazotambuliwa na Serikali.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa, baadhi ya wafanyabiashara wa Kitanzania waliojenga mtandao wao kwa baadhi ya maofisa wa Serikali, wameingizwa kwenye genge hilo na ndio ambao wamekuwa wakitumiwa kuwarubuni hadi kuwaibia wawezekaji.


Watanzania wanaotajwa kuwa wanachama wa genge la matapeli wa kimataifa, ni wamiliki wa migodi ya madini iliyo sehemu mbalimbali hapa nchini na wanatajwa kuwa na makazi ya kudumu katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Ruvuma.


Chano mtanzania gazeti augost26

0 comments: