Friday, 23 August 2013

MAUJI NA AJARI ZATOKIA MBEYA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

  HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 23. 08. 2013.

(DIWANI ATUMANI – ACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


WILAYA YA  KYELA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA  SAA 00:30 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA 70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA  KUPIGWA JIWE UBAVUNI NA ANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  KUKAA MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  MOMBA – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU                     NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA  SAA 05:30 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,  JINSI YA  KIUME MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA  TUKIO. . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed by:
(DIWANI ATUMANI – ACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments: