Wednesday, 7 August 2013

ANGARIA PICHA ZA UWANJA WA NDEGE JOMOKENYATA ULIVYO UNGUA MOTO NA CHANZO CHA MOTO HUO



JKIAPicture
  Moto ukiwaka JKIA Agosti 7, 2013. Picha/HISANI 
Imepakiwa - Wednesday, August 7  2013 at 

Wazimamoto kutoka KDF, Kaunti ya Nairobi na Kampuni za kibinafsi walifanikiwa kuzima moto huo baada ya masaa karibu manne. Chanzo chake bado hakijabainika.
Rais Uhuru Kenyatta alizuru eneo la mkasa mwendo wa saa tatu asubuhi lakini akaondoka bila kusema lolote.

Katibu wa Wizara ya Masuala ya Ndani Mutea Iringo amewashauri waliopanga kusafiri kupitia uwanja wa huo kuwasiliana na mashirika ya ndege husika.
Shirika la Msalaba mwekundu lilisema mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege la Kenya Airways na abiria wameathiriwa na moshi na kukimbizwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu.


Mkasa huo umetokea siku moja tu baada ya shughuli kutatizika kutokana na kukosekana kwa mafuta ya ndege jambo lililopelekea safari nyingi kukatizwa na ndege kulazimika kutua viwanja vingine jirani.
Waziri wa Uchukuzi Michael Kamau alisema ni mapema sana kusema uwanja huo utafunguliwa lini.
“Siwezi kusema uwanja wa JKIA utafunguliwa tena lini. Ni mapema sana. Chanzo cha moto hakijajulikana. Uchunguzi unaendelea,” akasema.
Bw Kamau aliwataka watu wasifunge safari kuelekea uwanja huo wa ndege ila tu vikosi vya kutoa huduma za dharura na wazimamoto.

Usalama
Waziri wa Usalama Joseph ole Lenku alisema usalama umeimarishwa na kuwataka wananchi na wageni wasiwe na wasiwasi.
“Mnaweza kuona vikosi vilivyofika hapa, ardhini na angani kuhakikisha eneo ni salama na anga pia. Hili linafaa kutosheleza Wakenya na wageni kwamba usalama wao unahakikishwa.  Hatukusudii kuufunga muda mrefu lakini lazima tuhakikishe usalama. Tunaelewa umuhimu wa uwanja huu kwa taifa.


“Tunazima moto na pia kupunguza hasara kuhakikisha hauathiri uchumi sana.”
Afisa Mkuu Mtendaji wa Kenya Airways kupitia taarifa kwa vyombo vya habari alisema abiria wote wa shirika hilo wako salama.
“Tungependa kuwajulisha wateja na wadau kwamba abiria waliokuwa wakiwasili JKIA na waliokuwa wakiondoka wako salama,” akasema.


Alieleza kuwa ni dhahiri kwamba shughuli zitatatizika lakini akasema maelezo mengi yatatolewa baadaye.
Ndege tano za shirika hilo zilizopangiwa kutua JKIA zimehamishiwa uwanja wa ndege wa Moi, Mombasa na wale waliokuwa safarini kuelekea viwanja vingine kupitia Nairobi wamepelekwa mahotelini.
Ndege zilizoelekezwa Mombasa ni KQ117, KQ331, KQ311, KQ863 na KQ203.

swahilihubblog
Imepakiwa - Wednesday, August 7  2013 at

0 comments: