Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Nalicho(Picha na Maktaba)
------------------------------ ------------------------------ ---------------
Na Steven Augustino wa Demashonews , TunduruMKUU wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Chande Nalicho amewataka
vijana kujenga tabia ya kujitokeza na kupata mafunzo ya Ulinzi wa nchi
yao ambayo yamekuwa yakitolewa katika maeneo yao kupitia proglamu ya
mafunzo ya jeshi la akiba la Mgambo
.
Dc, Nalicho alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya Jeshi la Ulinzi
la Mgambo yanayoendelea katika Tarafa ya Lukumbule Wilayani humo na
kwamba mbali na vijana hao kupatiwa mafunzo hayo ya ukakamavu lakini
pia hupatiwa mbinu za kuwakabili maadui wa nchi yetu.
Akifafanua taarifa hiyo Dc, Nalicho alisema kuwa endapo kundi hilo
litategea katika ulinzi wa nchi yao ni sawa na kukubali kuiweka rehani
nchi yao na kuiacha ichukuliwe na wanyang’anyi huku wao wakibakia kuwa
watazamaji.
Aidha Dc, Nalicho akaendelea kuwatia moyo wapiganaji hao wa Jeshi la
akiba kuwa ujuzi watakao upata kupitia mafunzo hayo pia yatawawezesha
kufungua ukurasa mpya utakao wawezesha kupata pia ajira hasa wakati
huu ambao makampuni mengi yatafunguliwa baada ya Wilaya yao kufunguka
kwa kuunganishwa na Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupiti ujenzi wa
Barabara ya Lami.
Awali afisa tarafa wa Lukumbule Godfrey Manyahi alimweleza Mkuu wa
Wilaya huyo kuwa pamoja na kupelekwa kwa fulsa hiyo Katika Tarafa yake
Vijana hao hawajaonesha moyo wa kushiriki katika mafunzo hayo na
kwamba hata 49 waliojitokeza na kuandikishwa nao pia wamekuwa watoro
wa kuhudhulia mafunzo hayo.
Manyahi alioendelea kueleza kuwa wanao hudhulia ni chini ya idadi
hiyo ambapo kati yao wasichana ni 2 tu kati ya Vijana zaidi ya 100
waliotarajiwa, idadi ambayo alisema kuwa ni ndogo mno ikilinganishwa
na mahitaji ya askari wa jeshi hilo katika tarafa yao iliyo mpakani
mwa nchi jirani ya msumbiji.
Alisema hivi sasa kumbukumbu za ofisi ya Tarafa hiyo zinaonesha kuwa
imebakia na hazina ya asikali mgambo wawi (2) tu ambao walipatiwa
mafunzo ya mwisho miaka 28 iliyopita yaliyofanyika mwaka 1985 nakwamba
hivi sasa ni Wazee hali inayo onesha uwepo wa umuhimu kwa Vijana hao
kujitokeza kwa wingi kwani mafunzo mengine kama hayo pia watachukua
muda mrefu kuwafikia tena katika maaeneo yao.
Akitoa taarifa ya mafunzo hayo Mshauri wa mgabo wa Wilaya ya Tunduru
Benedikti Komba aliwataka viongozi wa Tarafa hiyo kuto watumia vibaya
askari wanaotoa mafunzo hayo kwa vijana wao ili kuwawezesha kushirika
kikamirifu katika zoezi hilo.
Alisema Mafunzo hayo yatakayo dumu kwa kipindi cha miezi mitatu idara
yake imepeleka askari wakakamavu na wenye uzoefu mkubwa katikautoaji
wa mafunzo ya aina hiyo na akatumia nafasi hiyo kuwahimiza Vijana
ambao walianza kuregalega katika ushiriki wao kutokana tama na kwa
wanaohitaji waende na kuungana na wenzao kwani vijana wake wapo tayali
kuanzisha kikosi cha pili ili kuongeza idadi ya wahitimu.
0 comments:
Post a Comment