Monday, 26 August 2013

KILICHOKUTWA KWENYE KANISA LA KKKT SI BOMU POLISI YASEMA

Picture
Picha ya transfroma iliyopo KKKT-Kijitonyama na kitu kinachoning'inia ambacho polisi walikichukua ili kukichunguza
HOFU YA BOMU KANISANI, Dar es Salaam: Polisi jijni Dar es Salaam imetoa taarifa za awali za kifaa kilichokuwa kwenye transfoma iliyopo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Kijitonyama kwa kusema kuwa kitu hicho siyo bomu.kwa uchunguzuzi awali hayo yamesemwa na polisi baada ya kufika kwenye tukio hilo hapo jana  na Uchunguzi zaidi unaendelea.

---

VIONGOZI WA CHADEMA WASHIKILIWA NA POLISI NA KUHOJIWA, Iringa: Polisi mkoani Iringa Jana
asubuhi waliwakamata viongozi watano wa CHADEMA kwa tuhuma za kuzidisha muda wa kuhutubia katika mkutano wa hadhara kuhusu Mabaraza ya Katiba Mpya, uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi, amewataja waliokamatwa kuwa ni Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Joseph Mbilinyi, Mch. Peter Msigwa na Frank Nyalusi.

Kamanda Mungi alisema CHADEMA ilikuwa na kibali cha kuendesha mkutano tangu alasiri saa tisa hadi saa kumi na mbili jioni lakini mkutano huo uliendelea kwa nusu saa zaidi na kila mara walipokumbushwa kuhusu muda, walitoa maneno ya kuwakejeli Polisi hivyo ili kuepusha purukushani na vurugu, Polisi hawakuwakamata wakiwa jukwaani ila waliwafuata na kuwatia mbaroni asubuhi ya leo.

Viongozi hao wameachiliwa baada ya kushikiliwa kwa saa 16 na kupata dhamana ya shilingi milioni mbili kwa kila mmoja.

Source:
HABARI YA TBC TAIFA YATRH 25

0 comments: