Saturday, 31 August 2013

HIVYO NDIVYO CHEKA ALIVYO AMCHAPA MMAREKANI NA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA (ANGALIA HAPA PICHA)

 

CHEKA Vs WILLIAM...
NYOMI LA DIAMOND, LAKINI KUNA TAARIFA PROMOTA AMEAMBULIA PATUPU KUTOKANA NA KUGUNDULIKA KULIKUWA NA TIKETI FEKI KIBAO.

MMAREKANI ALIKAA KATIKA RAUNDI YA TATU...AKAINUKA NA KUENDELEA



Francis Cheka ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza Mtanzania kumtandika Mmarekani katika mchezo wa kuwania taji.

Cheka amefanikiwa kutwaa taji la dunia linalotambuliwa na WBF katika uzito wa Middle baada ya kumchapa bondia Phill Williams kutoka Marekani katika pambano lililomalizika punde kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.

Cheka amefanikiwa kushinda kwa pointi baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi wa ponti kwa kwanza akimpa 116-113, wa pili, 109-108  na wa tatu 117-111.


Pambano hilo lilikuwa kali na la kuvutia na mabondia walilianza kwa umakini mkubwa huku kila mmoja akionyesha kumsoma mwenzake hadi lilipochanganya kadiri raundi zilivyokuwa zinasonga mbele.


Baada ya Cheka kutangazwa bingwa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyekuwa mgeni rasmi alimvisha mkanda huo baada ya kutambulishwa na bondia mkongwe, Botha kutoka Afrika Kusini.


Kabla ya hapo, Thomas Mashali naye alifanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika baada ya kumchapa Mada Maugo kwa pointi huku majaji wakimpa ushindi wa 95-94, 95-95 na 95-94.


Pambano lilikuwa kali sana hali iliyofanya iwe kazi ngumu kwa mashabiki kutabiri nani ameibuka na ushindi hata baada ya raundi zote 10 kumalizika.


Pambano lingine lisilo la kuwania mkanda kati ya Alphonce Mchumiatumbo dhidi ya Chupaki Chipindi ambalo lilikuwa ni la uzito wa juu kabisa.


Mchumiatumbo alishinda kwa TKO katika raundi ya tano, ikiwa imebaki moja tu pambano hilo kumalizika na wasaidizi wa kona ya Chipindi wakaamua kutupa taulo.


Classic Mawe na Simba wa Tunduru ndiyo walianza kufungua ngumi za utangulizi na mwisho mkongwe Simba wa Tunduru akakubali matokeo kutoka kwa kijana huyo anayetokea Gym ya Ilala chini ya mwalimu wake Super D.

0 comments: