Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM, Millard Ayo akizungumza mbele
ya vijana wenzake, namna alivyobahatika kuzitumia fursa mbalimbali
alizokuwa akizipata kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mpaka hapo alipo,
anabainisha kuwa kilichompelekea hapo alipo mpaka sasa ni namna
alivyojijenga kwa nidhamu, kujituma na bidii kubwa ya kazi kila
alipokuwa akiipata fursa, aidha amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya
kukata tamaa mapema na kutokuwa wavivu wa kufanya kazi, kwani kwa
kufanya hivyo maendeleo hayatapatikana kirahisi.
Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar, Bwa.Salim
Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwa mtu yeyote
anayejiunga na shirika la NSSF, alifafanua hayo leo kwenye ukumbi wa
Luluma, nje kidogo ya mji wa Singida, Salim alibanisha kuwa mtu yeyote
atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la
matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika
hilo.Semina hiyo ambayo inafanyika ikiwa ni mkoa wa tatu huu, ikianzia
Kigoma, Tabora na sasa Singida, iliandaliwa na Clouds Media Group na
kufadhiriwa na shirika la NSSF, Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.
Sehemu washiriki wa Semina ya Fursa kwa vijana, wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo, ambayo
imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida
waliojitokeza kushiriki.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba, akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya
ukumbi wa Luluma, nje kidogo ya mji wa Singida, kuhusiana na fursa
mbalimbali wanazozipata vijana na kuhakikisha wanazitumia ipasavyo,
aliongeza kuwa vijana wengi wamekuwa ni watu wa kulalamika lalamika tu
na kukata tamaa mapema, aidha Ruge amewataka vijana kuwa na muamko wa
kufanya kazi na kujituma kwa bidii pale fursa yoyote inapotokea.
Kwa picha zaidi, tembelea MichuziJr.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment