Taarifa via JamiiForums na HabariLeo —
Basi la Meridian ililokuwa na abiria 60 likitokea Tarakea, Rombo,
mkoani Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam lilipata jali jana kwenye eneo
la Kimange, Mbwewe, mkoani Pwani na kusababisha vifo vya watu wawili
huku wengine 40 wakiachwa na majeraha mbalimbali katika miili yao.
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, shirika linalosimamia Hospitali ya Tumbi, Dk Cyprian Mpenda alithibitisha kuwa watu wawili walikufa katika ajali hiyo na kuwataja kuwa ni Gerald Laswai (43) na Musin Mwaliko ambaye umri wake haujafahamika. Aidha, Dk Mpenda alisema katika Hospitali ya Tumbi, walipokea maiti hao wawili na majeruhi 22, mchana jana, ambapo 12 ni wanawake na 10 ni wanaume na majeruhi mmoja kati ya hao, yuko mahututi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema jana kuwa, ajali hiyo ilitokea saa 5.40 asubuhi baada ya dereva aliyefahamika kwa jina moja la Rajab akiendesha basi hilo lenye namba za usajili T956 ABX kushindwa kulihimili gari kutokana na mwendo kasi baada ya kugonga kigingi na gurudumu kupasuka.
Kamanda Matei alisema katika eneo la tukio, hakukuwa na mtu aliyekufa lakini majeruhi walikuwa 40 na watu 20 walitoka wazima. Alisema majeruhi wengine walipelekwa katika Hospitali ya Lugoba na Chalinze.

0 comments:
Post a Comment