Thursday, 15 August 2013

MFUGAJI AUA MKEWE KWA WIVU WA KIMAPENZI

 
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNtgLN-a6eKiYcTtvyhZCCiKMdibTF9uko2kW8SDdwaxV7ByTr4vyWvdwyQ4Ypew7x7Nt1JeLLwme1Dkm4aXUNgi4M2_1eu8-gN9SbA6qGn_ucEbiJy48dQeGU-0Adza1MSGkZZEryLDes/s400/beat1.jpg
 Huu ni moja ya ukatili kwa kina mama(Picha na maktaba)
--------------------------------------------------------------------
  Na Steven Augustino wa Demashonews  Namtumbo

Mfugaji wa Jamii ya Kisukuma anayeishi katika Kijiji cha Mtelamwahi
Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Maiko Sajini(24) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumuua Mkewake
kutokana na kilicho daiwa kuwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa
kimapenzi.


Shuhuda wa tukio hilo Anna Yohana ambaye ni mjomba wa Marehemu alisema
kuwa Marehemu Dagwanedi Jogi (22) alikubwa na makasa huo baada ya mumewe huyo kumtuhumu kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmojaKijijini hapo hali ambayo ilizusha mtafaruku huo kati ya wanandoa
hao.


Alisema siku ya tukio mumewe huyo alisafiri kwenda kijiji jirani na kwa kawaida yake huwa anarudi usiku wa manane kama alivyo fanya siku hiyo,lakini kila anapo rudi humkuta mkewe  akiwa amelala lakini cha kushangaza wakati akikaribia nyumbani hapo alikutana na kijana huyo
njiani ambaye kila mara alidai kuwa amekuwa akimhisi kumuiingilia
 

katika ndoa yake na hata alipofika nyumbani kwake alimkuta mkewe akiwa
hajalala hali amabyo ilimfanya amhoji juu ya hali hiyo.


Alisema wakiwa katika mahojiano hayo ilitokea kuto elewana kati yao
ambapo mwanaume huyo aliomba amkague mkewe huyo katika sehemu zake za
siri ili kujiridhisha juu ya mashaka yake hayo lakini marehemu
alikataa kata kata hali ambayo ilimfanya mtuhumiwa huyo kutumia nguvu
katika ukaguzi huo ambapo baada ya kuangalia aligundua kuwa mkewe huyo
alikuwa ametoka kufanya tendo hilo alilo lihisi.

 
Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kata ya Ligera Alli Manoni alisema
kuwa baada ya kupokea taarifa hizo yeye kwa kushirikiana na uongozi wa
Kijiji cha Mtelemwahi walienda eneo la tukio na kushuhudia unyama huo
lakini kwavile mtuhumiwa alikuwa amekimbia walitoa taarifa Polisi
ambao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anaelekea katika
Kijiji cha Suruti Wilaya ni humo.

 
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusidedith Nsimeki amedhibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani
kujibu tuhuma za mauaji hayo baada ya kukamilika kwa taratibu za
kipolisi.


Aidha Kamanda Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa pamoja na mambo
mengine Polisi wanaendelea kumsaka mtu ambaye alidai kuwa chanzo cha
ugomvi huo mabao ulisababisha mauaji hayo ambayo hadi sasa jina lake
halijafahamika.


Habari kwa hisani ya Demashonews

0 comments: