Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ya kuwavua
madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la polisi nchini na kumsimamisha kazi
mmoja kutokana na kukiuka maadili na taratibu za Jeshi la Polisi.
(picha: Lorietha Laurence – Maelezo)
Imeandikwa
na Lydia Churi —
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi
amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na
kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana
na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao.
Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013.
Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta Juma Mpamba na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya

Kasulu ASP Daniel Bendarugaho na kumsimamisha kazi Inspekta Isaack Manoni.
Alifafanua kuwa Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi.
Alisema askari hao wawili waliokamatwa wakisafirisha bangi, walikuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha Ngarananyuki na baada ya kukiri kosa walifukuzwa kazi mwezi Mei mwaka huu.
Alisema kwa upande wa Inspekta Jamal Ramadhan amevuliwa madaraka yake kwa kutochukua hatua stahiki baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara wa Mvomero Samson Mwita kubambikiwa fuvu la kichwa cha binadamu na askari polisi watatu wakishirikiana na matapeli wawili.
“Katika tukio hilo Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na atashtakiwa kijeshi kutokana na tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa, Cpl. Edward aliyekuwa dereva wa gari la Polisi lililokamatwa na bangi kitendo ambacho kimelifedhehesha jeshi la polisi” alisema Waziri Nchimbi.
Alibainisha kuwa Inspekta Juma Mpamba amevuliwa madaraka hayo kwa kuonesha udhaifu katika utendaji wake wa kazi kwa kutosimamia kikamilifu askari walio chini yake kitendo kilichosababisha askari kujipangia kazi nje ya utaratibu na kumbambikiza mfanyabiasha huyo kesi kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi. Aliongeza kuwa askari waliohusika na tukio hilo wamefukuzwa kazi na kushtakiwa.
Waziri Nchimbi alisema ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba aliyeuawa baada ya kupigwa na askari polisi wawili Desemba mwaka jana.
Alisema upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa upelelezi ulisababisha kesi hiyo kuondolewa mahakamani. Aliongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TAARIFA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YANCHI MHE. DKT. EMMANUEL J. NCHIMBI (MB)KWA VYOMBO VYA HABARI
UCHUNGUZI WA MATUKIO YALIYOLALAMIKIWA DHIDI YAASKARI POLISI KATIKA MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO,MOROGORO NA KIGOMA
Kati ya tarehe 26 Desemba 2012 na tarehe 18 Mei 2013, yametokea matukio mbalimbali katika Jeshi la Polisi yaliyolalamikiwa na wananchi na kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Baadhi ya matukio hayo ni yafuatayo:-
Tukio la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia kutumika katika uhalifu (ubebaji wa bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Polisi Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha.
Mauaji ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la Polisi.
Baada ya kuyapokea malalamiko hayo, niliunda Kamati ya kuyachunguza ili kubaini ukweli. Kamati imefanya kazi niliyowatuma na kunikabidhi Taarifa ya Uchunguzi. Baada ya kuipitia Taarifa hiyo kwa makini nimeridhia maoni ya Kamati na hivyo tumefanya maamuzi yafuatayo:
TUKIO LA BANGITukio hili lilitokea tarehe 18 Mei 2013 majira ya saa tano na nusu za usiku maeneo ya Kilema Pofu katika barabara ya Himo Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kufuastia tukio hilo, waliokuwa Askari Polisi Ex F.1734 Cpl Edward wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha na Ex G.2434 PC George wa Kituo cha Polisi Ngarananyuki, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha walifukuzwa kazi tarehe 20/05/2013 baada ya kukiri kosa la kusafirisha bangi kwa kutumia gari ya Polisi.
Katika tukio la gari lenye usajili PT 2025 Toyota Land Cruiser la Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha kutumika katika ubebaji wa bangi yenye uzito wa kilogramu 540 zenye thamani ya Tshs 81,000,000/= kukamatwa mkoani Kilimanjaro usiku wa tarehe 18 Mei, 2013, Mkuu wa Kikosi hicho Mkarakibu wa Polisi Ramadhan Giro amevuliwa madaraka aliyonayo kwa kushindwa kuwasimamia kikamilifu Askari na Maafisa walio chini yake na kusababisha hilo kutokea.
Kitendo cha Inspekta Isaack Manoni kutuhumiwa kumtorosha mtuhumiwa hatari Ex F.1734 Cpl Edward aliyekuwa dereva wa gari la Jeshi la Polisi lililokamatwa na bangi Mkoani Kilimanjaro ni cha kulifedhehesha Jeshi la Polisi. Hivyo, Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na nimeagiza ashtakiwe kijeshi.
Kitendo cha Inspekta Salum Juma Kingu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Kilimanjaro kubaki kwenye gari umbali wa mita 80 kutoka nyumba ya mtuhumiwa Ex F.1734 Cpl Edward wakati Cpl Edward alipokuwa amepelekwa kutoka Moshi kukabidhi vifaa vya Jeshi la Polisi, kilichangia mtuhumiwa kutoroka. Inspekta Salum Juma Kingu amepewa onyo na anatakiwa kuwa makini katika utendaji kazi wake.
Inspekta Mikidadi Galilima hakutimiza wajibu wake ipasavyo katika kumshauri Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha katika ukaguzi na usimamizi wa rasilimali za kikosi. Aidha, kitendo chake cha kujaribu kuficha ukweli kwa kuelekeza matairi mapya yaliyonunuliwa na Ex F.1734 Cpl Edward yavuliwe na yarejeshwe ya zamani kwenye gari PT. 2025 baada ya uhalifu ni cha kukosa uadilifu kama kiongozi. Inspekta Mikidadi Galilima amepewa onyo kali.
PF 15828 ASP Francis S. Duma aliyekuwa kiongozi katika tukio la kukamata gari ya Jeshi la Polisi lililokuwa limebeba bangi Mkoani Kilimanjaro amepandishwa cheo kuwa Mrakibu wa Polisi kuanzia jana tarehe 21/08/2013. Aidha, Askari 14 aliokuwa nao siku hiyo ya tukio wapongezwe kwa kupewa zawadi inayostahili ndani ya mamlaka ya IGP.
2.0 TUKIO LA FUVUTarehe 07 Mei, 2013 Askari watatu wa Jeshi la Polisi Ex E.4344 D/Sgt Mohamed na Ex E.3861 Cpl Nuran wa kituo cha Polisi Dumila na Askari Polisi Ex D.4807 D/SSgt Sadick Madodo wa kituo cha Polisi Dakawa wakishirikiana na raia wawili matapeli Rashid Hamis @ Shariff na Adam Peter @ Saloon walimbambikizia fuvu la kichwa cha binadamu mfanyabiashara Bw. Samson Mwita @Kihindi wa Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kupata fedha. Askari hao wamefukuzwa kazi na wameshtakiwa kwa uhalifu waliotenda.
Kabla ya tukio hili Inspekta Jamal Ramadhan ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mvomero alikuwa na taarifa ya mpango wa kufanyika utapeli katika maeneo ya Dakawa na Dumila ambapo matapeli walikuwa wanapanga kwa kushirikiana na Askari Polisi wasio waaminifu kuwabambikizia watu kesi kwa lengo la kupata fedha, lakini hakumtaarifu Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila. Aidha, Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila Inspekta Juma Mpamba ameonesha udhaifu katika utendaji kazi wake kwa kutosimamia kikamilifu Askari walio chini yake, kitendo kilichosababisha Askari hao kujipangia kazi nje ya utaratibu, hivyo kuwa na ujasiri wa kumbambikizia mfanyabiashara kesi kwa kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi.
Aidha, Inspekta huyu alishindwa kumfuatilia na kumkamata tapeli maarufu Bw. Adam Peter @ Saloon aliyekuwa kinara wa tukio hili hadi Kamati ilipotoa msisitizo na shinikizo la kukamatwa kwa tapeli huyo. Kutokana na kasoro zilizoainishwa dhidi ya Inspekta Jamal Ramadhan na Inspketa Juma Mpamba, wote wamevuliwa madaraka walionayo.
3.0 TUKIO LA KASULUTarehe 25 Disemba, 2012 usiku wa kuamkia tarehe 26 Disemba, 2012 katika Kituo Kidogo cha Polisi Heru UShingo kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Askari Polisi Ex D.8622 Cpl Peter na Ex G.1236 PC Sunday kwa pamoja walimpiga marehemu Gasper Mussa @ Sigwavumba mwenye umri wa miaka 36 na kisha kumweka katika Mahabusu ya Kituo hicho bila msaada wowote wa matibabu hatimaye kufariki tarehe 26 Disemba, 2012 majira ya asubuhi kutokana na kupasuka kwa bandama. Upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho katika kesi ya mauaji dhidi ya Askari hao ambao tayari walikuwa wameshafukuzwa kazi ulisababisha kesi kuondolewa Mahakamani.
Kutokana na kitendo cha Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa jalada husika la kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba; ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka aliyonayo. Aidha, upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.
Dkt Emmanuel J. Nchimbi (MB)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
22/08/2013

0 comments:
Post a Comment