Friday, 30 August 2013

BAN KI MOON ALAANI KUUAWAWA KWA MLINZI WA AMANI WA TANZANIA DRC

Picture
Walinzi wa Amani wakiwa katika moja ya doria kwenye mitaa ya mji wa Goma
Imeandikwa na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon  amelaani kuuawa kwa Mlinzi wa Amani kutoka Tanzania  ambapo wengine  kadhaa  wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na   kundi la waasi la M23 katika  katika  eneo la Mashariki ya   Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa   na msemaii wa Katibu Mkuu ,  inaeleza kwamba. “ Katibu Mkuu analaani kwa nguvu zote mauaji  ya mlinzi huyo na  kujeruhiwa kwa walinzi  wengine  10 na anatoa salamu zake za rambirambi kwa familia  za walinzi hao  na  kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Jamhuri ya Afrika ya kusini”.

Mashambulizi dhidi ya walinzi hao wa Amani yametokea   siku ya  jumatano katika  Vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu ambako Misheni ya   kutuliza Amani   ya  Umoja wa Mataifa katika DRC ( MONUSCO)  ilikuwa ikisaidiana  na majeshi ya  serikali ya   DRC kuwalinda raia katika eneo  la Goma ambalo lina idadi kubwa ya watu.

Kwa mujibu wa taarifa  hiyo,  MONUSCO  ilijibu mashambulizi hayo kwa kutumia zana mbalimbali za kivita yakiwamo makombora, mizinga na helkopta za kivita wakati majeshi ya DRC yalitumia askari wa ardhini,  vifaru

Chanzo wavutiblog

0 comments: