Bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla ‘Snake Man’ ametakiwa kuachana na ngumi mara
moja na ikiwezekana astaafu kabisa.
Maagizo hayo
yametoka kwa mmoja wa madktari wanaoshughulikia masuala ya michezo nchini.
Akithibitisha
suala hilo, Matumla ,44, amesema daktari huyo amemueleza kuachana na mchezo wa
ngumi kama mchezaji na badala yake anaweza kuwa mwalimu kwa kuwa afya yake
haimruhusu.
“Kweli huyo
daktari ambaye nisingependa kumtaja ameniambia hilo, alisema hayo baada ya
kunifanyia vipimo.
“Unajua kwa
muda mrefu nimekuwa nikusumbiliwa na matatizo ya mgongo. Sasa vipimo
vinaonyesha nina matatizo kidogo.
“Hata baadhi
ya viungo vyangu vimekuwa havifanyi kazi vizuri kama ilivyokuwa awali,”
alisema.
Kuhusiana na
kama kweli yuko tayari, Matumla ambaye amewahi kutangaza anastaafu na baadaye
akarejea, alisema: “Kweli nahitaji kufanya hivyo, lakini naupenda mno mchezo wa
ngumi hadi nachanganyikiwa.
0 comments:
Post a Comment