Tuesday, 6 August 2013

TASO YAGOMEA SERIKALI KUAHIRISHA SHEREHE ZA NANENANE KUPISHA SIKUKUU YA IDDI.


Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe 
Siku chache zikiwa zimebaki ili kufikia kilele cha maadhimisho ya s kumeibuka mgongano  baina ya Chama cha wakulima (TASO)na serikali kuhusu maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7au 8, mwaka huu.

Mgongano huo umekuja baada ya serikali kutaka maadhimisho hayo yafanyike  Agosti  7 mwaka huu huku chama cha wakulima kikiweka msimamo wake wa kusherehekea  maadhimisho hayo agosti,  8 mwaka huu .

Akizungumza jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Mwenyekiti wa Chama cha wakulima (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini,Kapten Mstaafu Noel Nkoswe wakati wa majumuisho na waandishi wa habari baada ya kuibuka vuta nikuvute  na serikali  kuhusu kilelele cha maadhimisho hayo ya wakulima.

Kapten Nkoswe amesema kuwa wao kama chama cha wakulima msimamo  wao upo pale pale wa sherehe hiyo  ya wakulima kufanyika Agosti 8 mwaka huu kama ilivyopangwa kila mwaka.

Amesema Wakulima wao  lazima l washerekee sikukuu yao kama kawaida  hivyo mpango wa kubadilisha tarehe  haupo ambapo chama hicho kwa msimao wake kitafanya   tarehe 8 na zawadi za wakulima kutolewa   agosti 8 kama ilivyo pangwa.

        Kapten mstaafu Nkoswe  amesema mwenyekiti wa TASO taifa aliyemtaja kwa jina moja amemwelekeza kuwa maadhimisho ya kilele cha sikukuu hiyo yatafanyika kitaifa katika kanda ya kati Dodoma Agosti 7 mwaka huu ambapo katika kanda zingine zitafanya kama kawaida Agosti 8 mwaka huu.

Hata hivyo  kwa upande wake Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa wamepokea barua ya serikali inayotaarifu sherehe za kilele cha nane nane zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na sikukuu ya Idd kuwa agosti 8 mwaka huu .

Hata hivyo katika barua iliyotumwa na wizara ya kilimo chakula na ushirika yenye kumbu kumbu namba AE 18/196/01 ya julai 30 mwaka huu  kwenda kwa waziri wa nchi sera uratibu na bunge ofisi ya waziri mkuu iliyoandikwa  na waziri wa kilimo na chakula Eng Christopher Chiza  na nakala kwa wakuu wa mikoa yote minne ya kanda ya nyanda za juu kusini.

Aidha nakala ya barua hyo iliyotumwa kwa katibu mtendaji Taifa  imesema kuwa  sherehe za kilele cha nane  nane  imeamliwa zifanyike Agosti 7 mwaka huu  kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Idd ambapo Waziri wa nchi Mh.William Lukuvi  atakuwa mgeni rasmi katika sherehe  hizo.

NA mbeya Yetu Blog

0 comments: