Monday, 5 August 2013

MASHINDANO YA KUSOMA NA KUHIFADHI QUR ANI MKOA WA MBEYA YA FANIKIWA VEMA


Mtoto Habibu Abdulrahman(8) ambaye amehifadhi juzuu ya kwanza akionesha umahiri wake wa kuhifadhi na kusoma Koran katika mashindano yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya jana mchana, Abdulrahman amekuwa mshindi wa kwanza kwa kusoma na kuhifadhi koran juzuu moja.



Mtoto Abubakar Muharram(12) akionesha umahiri wa kusoma Koran na kuhifadhi Juzuu saba wakati wa mashindano ya yaliyofanyika Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya, Abubakar amekuwa mshindi wa kwanza katika kundi la wanafunzi waliojitokeza kusoma na kuhifadhi Juzuu Saba amepewa zawadi ya Msahafu maalum unaotumia umeme na fedha taslimu Sh.80,000


Majaji wakifuatilia kwa makini mashindano ya kusoma Koran kabla ya kupatikana washindi


Mgeni rasmi Shekh Said Jabir pamoja na baadhi ya maimamu wakifuatilia mashindano hayo


Majaji wakiwa kazini kumtafuta mshindi




Mgeni rasmi Shekhe Said Jabirakitoa nasaha kabla ya kupatikana kwa mshindi


Mgeni rasmi akimpa mkono mmoja wa majaji wa mashindano hayo Shekhe Abbas Mshauri






Mgeni rasmi akimpongeza mshindi wa kwanza wa kusoma na kuhifadhi Koran na Juzuu moja

Mshereheshaji wa mashindano hayo Shekhe Ibrahimu Bombo akiwaongoza wasomaji na wahifadhi wa Koran


Mshindi wa kwanza wa kusoma Koran juzuu saba Abubakar Muharam akiwa na msahafu wake wa Digital


 Baadhi ya waumini na wanafunzi wa madrasa mbalimbali waliohudhuria mashindano ya kusoma Koran
Picha zote na  Rashid Mkwinda 

0 comments: