Ofisa
Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda, amewavua madaraka Mratibu wa
Elimu Kata ya Chemba, Valentino Kisuja na Mussa Lali aliyekuwa Mkuu wa
Shule ya Sekondari Changaa kwa kushindwa kuwajibika.
Hayo yalitokea hivi karibuni wakati wa ziara ya ofisa huyo ambaye aliwataka walimu wakuu wa shule za sekondari na msingi kuondokana na dhana potofu kuwa kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani hapa kunatokana na mwamko duni wa elimu kwa wazazi: “Kutokana na kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani hapa nimewavua madaraka baadhi ya watendaji ili liwe fundisho kwa wengine,” alisema Kaponda.
Kaponda amesema amebaini kwamba walimu hawafundishi ipaswavyo, hali iliyosababisha kukithiri kwa utoro wa wanafunzi na kuporomoka kwa elimu. ---

Hamida Ramadhan, TANZANIA DAIMA, Kondoa.
0 comments:
Post a Comment