Wafanyakazi wametakiwa kuwa na mshikamano katika sehemu zao za kazi ili kuongeza ufanisi wa kazi maofisini.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa viwanda, biashara, tasisi za
fedha, huduma na ushauri (TUICO) Nyanda za juu kusini Bwana Merboth Kapinga
walipokwenda kutembelea mgodi wa Mtera.
Bwana
Kapinga amewaambia wajumbe wa chama cha wafanyakazi kuwa nguvu ya chama ni
wafanyakazi wenyewe kushirikiana kwa pamoja na kuzilinda mali za maofisini
mwao.
Katibu wa chama cha
wafanyakazi(TUICO) Nyanda za Juu Kusini Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na
wafanyakazi Walipotembelea bwawa la Mtera.
Aidha
Bwana Kapinga amewataka wakuu wa idara kuwaelimisha wafanyakazi juu ya umuhimu
wa kazi zao pia amewataka wafanyakazi wa ngazi za chini kukaa kikao na kujadili
na kutoa mawazo tofauti tofauti kwa wakuu wa idara ili yaweze kupelekwa kwenye
ngazi za juu.
Hata
hivyo wafanyakazi walitembelea bwawa la Mtera walifurahishwa na ziara hiyo
iliyowapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuilinda na kuliendeleza taifa la
Tanzania.
Kaimu meneja wa tanesco
tawi la Mtera Ndugu Salum Omar Njipwili akitoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa
Nyanda za Juu kusini.
Wafanyakazi kutoka
nyanda za juu kusini na tawi la tanesco Mtera wakisikiliza kwa makini kikao cha
viongozi wa TUICO.
Pia
wafanyakazi wa tanesco wakishirikiana na Kaimu Meneja wa Tanesco tawi la Mtera Bwana
Salum Omar Njipwili walifurahishwa na
ujio wa wafanyakazi kutoka nyanda za juu kusini hivyo wamewataka kuja
kutembelea mara kwa mara ili kujifunza mambo mengi zaidi.
Wafanyakazi wa Nyanda
za Juu kusini wakiwa na wafanyakazi wa Tanesco tawi la Mtera katika picha ya
pamoja.
NA
DIANA BISANGAO WA IRINGA
0 comments:
Post a Comment