>>WACHAMBUZI WADAI: “TATIZO NI KUBADILI TIMU KILA MECHI NA KUBADILI WACHEZAJI SHAGALABAGALA KWENYE MECHI!”
>> REKODI BAADA REKODI ZAPOROMOKA CHINI YA MOYES!!
WAKATI Meneja wa Manchester United, David Moyes, akidai walikosa bahati na ndio maanawakafungwa
2-1 hapo Jana na Stoke City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, hicho
kikiwa kipigo cha 8 kwenye Ligi msimu huu, baadhi ya Wachambuzi wamedai
tatizo kubwa la Man United hivi sasa, ukiondoa kuandamwa na Majeruhi, ni
kubadili Kikosi katika kila Mechi na pia kukosa umakini wa kubadilisha
Wachezaji wakati wa Mechi.
Stoke walishinda kwa Bao mbili za
Charlie Adam, la kwanza likiwa ni Shuti lake kumbabatiza Michael Carrick
na kutinga, na licha ya Robin van Persie kuisawazishia Man United, Adam
tena alipiga Bao la pili kwa Shuti la mbali.
TAKWIMU ZA MECHI:
Stoke vs Man United:
MASHUTI: Stoke 13 Man United 19
MASHUTI YALIYOLENGA GOLI: Stoke 6 Man United 4
MASHUTI NJE YA GOLI: Stoke 6 Man United 7
MASHUTI YA LIYOZUIWA: Stoke 1 Man United 8
PASI: Stoke 268 Man United 441
UMILIKI MPIRA: Stoke 38% Man United 62%
Katika Mechi hiyo Man United walipata
bahati mbaya kwa kuwapoteza Masentahafu wao wote wawili walioanza Mechi
hiyo pale Jony Evans alipotolewa katika Dakika ya 10 baada kuumia na
nafasi yake kuchukuliwa na Rafael huku Smalling akitoka Fulbeki na
kwenda Sentahafu lakini baada kuumia Phil Jones, aliekuwa akicheza
Sentahafu, Moyes aliamua kumuingiza Straika Danny Welbeck kuchukuwa
nafasi yake na kumrudisha Kiungo Michael Carrick kuwa Sentahafu huku
Rooney akishuka Kiungo.
REKODI BAADA REKODI ZAPOROMOKA CHINI YA MOYES:
-Stoke wanapata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Man United tangu 1984
-Swansea wanashinda Gemu ya kwanza Old Trafford
-Newcastle wanashinda mara ya kwanza Old Trafford tangu 1972
-Everton wanashinda mara ya kwanza Old Trafford tangu 1992
-West Brom wanashinda mara ya kwanza Old Trafford tangu 1978
Uamuzi huo wa Moyes uliwaacha Wachambuzi
wengi midomo wazi maana wao na Watu wengi walitegemea kurudi kwa
Carrick kuwa Sentahafu ingepaswa aingizwe Kiungo ambapo kwenye Benchi
alikuwepo Darren Fletcher ambae kwenye Mechi zote alizocheza ameonyesha
kiwango kizuri tu.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Moyes alisema: “Sijui hata tufanye nini ili tushinde. Nadhani tulikuwa na bahati mbaya mno.”
0 comments:
Post a Comment