Mwigizaji
wa filamu Jacob Steven JB akizungumza kwa niaba ya wenzake kabla ya
waigizaji hao wa Bongo Movie kukabidhiwa kadi zao na Rais Jakaya Kwete
kwenye uwanja wa Sokoine leo
Mwigizaji
wa filamu Jacob Steven JB akizungumza kwa niaba ya wenzake kabla ya
waigizaji hao wa Bongo Movie kukabidhiwa kadi zao na Rais Jakaya Kwete
kwenye uwanja wa Sokoine leo, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC
Siasa,Itikadi na Uenezi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akikabidhi bajaji kwa mmoja wa walemavu ambaye alimuahidi kumpatia bajaji hiyo. mMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete aki
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na wasanii waigizaji wa
filamu mara baada ya kuwakabidhi kadi zao kwenye uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya leo
SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM KATA YA MABATINI WAITAKA SEREKALI KUKEMEA MAOVU
Mahmoud Ahmad Mwanza
Serekali
imetakiwa kukemea maovu na ufisadi ili wananchi wawe na imani na chama
chao na serekali iliyo madarakani kwani bila kukemea maovu yanayotokana
ubadhirifu wa mali za serekali kwa waliopewa dhamana kujali mifuko yao
badala yawalio wengi itazidi kukiumiza chama nakushindwa kukiamini kuwa
kinatetea wanyonge.
Akizungumza
kwenye kilele cha madhimisho hayo kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa
chama wa kata hiyo katibu wa CCM wa kata ya Mabatini Gerald Mashala
alisema kuwa kumekuwa na kawaida kwa watendaji wa serekali wasio
waminifu kufuja mali za umma na kwataka viongozi wa chama hicho
kuendelea kukemea maovu sanjari na ufisadi bila kmuonea haya yeyote
kwani sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza serekali
Mashala
pia aliwataka wakazi wa jiji la mwanza na Tanzania kwa ujumla kuacha
kutoa malalamiko pekee yake kwani hayasaidi katika ujenzi wa taifa na
badala yake wajitume kuliletea maendeleo taifa lao huu ndio uzalendo wa
kweli malalamiko pekee hayasaidi tunatakiwa kukemea kwa nguvu zetu zote
kila aina ya maovu na ufisadi.
”
Utaifa kwanza ndio silaha yetu katika kujikomboa kutokana na maovu na
ufisadi uliokithiti kwenye idara za serekali kwani malalamiko pekee
hayatatasaidia kuondokana na maovu na ufisadi hapa tupige vita kwa nguvu
zetu zote” alisisitiza Mashala.
Nae
mwenyekiti wa ccm wa kata hiyo Yasiry Fuad aliwataka watanzania kuwa na
mshikamano wakati huo tunapoelakea kwenye bunge la katiba nakuondoa
itikadi za kisiasa na kuvaa utaifa kwani katiba si ya kisiasa inahitaji
uzalendo wa hali ya juu katika kufikia mmustakabali wa taifa letu.
Fuad pia alisema kuwa suala la kukemea maovu ni jukumu letu
sote na kuwataka watazania kujenga utamaduni wa kukemea maovu bila
kujali itikadi za kisiasa kwani maendeleo hayana itikadi tuwe pia na
tabia ya kujituma ilikujiletea maendeleo endelevu nakuacha malalamiko
kwani serekali haiwezi kukuletea maendeleo nyumbani pako inainaleta
maendeleo kwa jamii nzima.
0 comments:
Post a Comment