Sunday, 2 February 2014

KERRY KUKUTANA NA UPINZANI WA UKRAINE UJERUMANI

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani  Frank-Walter Steinmeier akimkaribisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika uwanja wa ndege wa Berlin kwa ajili ya mkutano huko Berlin, Jan. 31, 2014.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akimkaribisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika uwanja wa ndege wa Berlin kwa ajili ya mkutano huko Berlin, Jan. 31, 2014.
 
Maafisa wa Marekani wanasema waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry atafanya mkutano wake wa kwanza na wapinzani wa Ukraine ambao walikuwa wakiongoza maandamano ya kupinga serikali nchini humo tangu mwezi Novemba.

Kerry kwenye ziara yake Ujerumani atafanya mazungumzo Jumamosi na mwanasiasa wa upinzani Arseny Yatsenyuk na bingwa wa zamani wa ndondi ambaye sasa amekuwa mwanaharakati Vitali Klitschko.


Wakati huo huo waandamanaji wa Ukraine walionyesha kukasirishwa baada ya mwanaharakati wa upinzani Dymtro Bulatov aliyepotea tangu January 22 kupatikana nje ya Kyiv alhamisi akiwa amechubuka na kuchanika usoni.Bulatov anasema alitekwa nyara na watu wasiojulikana na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya kutupwa msituni.Anasema alijongea kijiji cha karibu ambapo aliweza kuwapigia simu marafiki zake.


Ofisi ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu imemtaka rais wa Ukraine Viktor Yanukovych kuchunguza taarifa za hivi karibuni za vifo uteswaji  na utekaji nyara wakati wa ghasia za kisiasa nchini humo.Msemaji wa kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Navi Pillay amesema kamishna huyo amesikitishwa sana na ripoti hiyo.

0 comments: