MWAKA JANA
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela akitoa
taarifa za matukio ya ajali kwa mwaka 2013 kwa mwakilishi wa MOblog
mkoani Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA ya ajali 246 zimetokea mkoani Singida kwa kipindi cha mwaka jana na kati yake 116 zilisababisha vifo vya watu 129.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,
SACP, Geofrey Kamwela wakati akitoa taarifa yake ya hali ya uhalifu
mkoani humo kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana
(2013),
Amesema
idadi hiyo ya ajali ni ongezeko la matukio mawili ambayo ni sawa na
asilimia 0.8 ikilinganishwa na ajali zilizotokea mwaka juzi (2012).
Aidha,
Kamwela amesema katika ajali za mwaka jana,watu wapatao 299
walijeruhiwa ambapo idadi hiyo ni pungufu kwa asilimia 15,ikilinganishwa
na majeruhi 353 kwa kipinid cha mwaka juzi.
“Katika
kipindi hicho,makosa madogo madogo 22,584 yaliripotiwa ambapo watu
20,127 walikamatwa na kutozwa tozo ya zaidi ya shilingi 684.9.Kiasi
hicho ni ongezeko la shilingi 185.1 sawa na aslimia 37,ikilinganishwa na
kipindi kama hicho kwa mwaka juzi”,amesema.
Kuhusu
makosa ya jinai,Kamwela amesema jumla ya makosa ya jinai 11,101
yaliripotiwa na kati yake makosa makubwa yalikuwa 1,358 na madogo 9,743.
“Mwaka
juzi makosa ya jinai yalikuwa 12,042 yaliripotiwa, na makubwa yalikuwa
1,337 wakati madogo yalikuwa 10,705.Makosa hayo yakilinganishwa na ya
mwaka jana (2013),kuna upungufu wa makosa 941 ambayo ni sawa na aslimia
7.8”,amesema.
Wakati
huo huo,Kamanda Kamwela amesema katika makosa ya kuwania mali,jumla ya
mali yenye thamansi ya zaidi ya shilingi 707.8,zillibwa na mali yenye
thamani ya zaidi ya shilingi 231.2 iliokolewa.
Amesema jumla ya watu 577 walifikishwa mahakamani na kupewa adhabu za vifungo au kulipa faini mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment