NA DIANA
BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM,IRINGA
WATU
watano wanashikiliwa na polisi mkoani Iringa kwa makosa mawili tofauti likiwemo
la wakazi watatu wa dare s salaam kukutwa na pembe tano za ndovu maeneo ya
kijiji cha ngenza kata ya ikweha tarafa ya sadani wilaya ya mufindi..
Akizungumza
na mtandao wa www.matukiodaima.com
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa RAMADHANI MUNGI alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo lililotokea januari 11.
Hata
ivyo aliwataja watu hao ni RAJABU MARI (35), KADILI MOHAMED (27) na SALOME
ALOYCE(50) ambao walikuwa wakitumia gari aina ya premio lenye namba za usajili
T580 mali ya FROLIAN ELIUS mkazi wa Dar es S alaam walikutwa na pembe hizo
zenye uzito wa kilogramu 37 ambazo thamani yake bado haijafahamika.
Wakati
huohuo jeshi la polisi Iringa linawashikilia watu wawili majina RIZIKI KAFULILO
(24) na MIRAJI NZOWA (28) wote wakazi wa mashine tatu manispaa ya Iringa kwa
kosa la kukutwa na kete 16 za madawa.
MUNGI
alisema tukio hilo lilitokea mnano tarehe 12 januari mwaka huu maeneo ya kirabu
cha pombe za kienyeji ubena kata ya mivinjeni ambapo kete hizo zinazaniwa kuwa
ni madawa ya kulevya.
Aidha
kamanda MUNGI alithibitisha kutokea kwa tukio jingine la mkazi wa luhunga
tarafa ya ifwagi wilaya ya mufindi Jina JUSTINE LUWUNGO (22) ambaye ni mkulima
kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili
wake baada ya kuiba kuku.
0 comments:
Post a Comment