Na Gladness Mushi Arusha
………………………………………………………………
SERIKALI
imefanikiwa kutoa kiasi cha Bilioni moja na Milioni 750 kama fidia kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mara baada ya kuchukua mradi wa
Halmashauri hiyo ujulikao kama Laki Laki kwa ajili ya kujenga miji ya
kisasa zaidi.
Akidhibitisha
mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri mkurugenzi
mtendaji Bw Fidelis Lumato alisema kuwa mpaka sasa wameshapokea fidia
hiyo ya mradi wa mashamba ya Laki laki ambao ulikuwa chini ya
Halmashauri hiyo .
Lumato alisema kuwa pamoja na kuwa mpaka sasa wameshaweza
kuachia mradi huo na kutoa kwa Serikali kuu lakini fidia hiyo itasaidia
sana kuweza kufanya marekebisho ndani ya Halmashauri hiyo ikiwa ni
pamoja na kununua mahitaji ya msingi.
Alidai kuwa
fidia hiyo imeweza kurahisisha kazi mbalimbali za halmashauri kwa kuwa
yapo mahitaji ya msingi ambayo yalikuwa yanahitajika lakini hapakuwa na
jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kununua jambo ambalo wakati mwingine
lilikuwa linasababisha malengo kukwama.
Aidha
alitaja vitu ambavyo vitaweza kununuliwa kutokana na fidia hiyo kuwa ni
pamoja na Gari kwa ajili ya matumizi ya shule za sekondari katika
Halmashauri hiyo,tipper kwa ajili ya shuguli za ujenzi ambapo pia nalo
litachangia mapato ya halmashauri hiyo.
Vitu vingine
ambavyo vitafanyika kutokana na fidia hiyo ni pamoja na ukarabati wa
jengo la kisasa la Halmashuri hiyo ambalo bado halijaweza kukamilika
rasmi kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri hiyo.
“tunashukuru
mungu serikali kutupa fidia ya mradi wa mashamba ya Lakilaki kwani kwa
kipindi cha mwaka huu tutafanya vitu vingi na tunaimani kabisa hata
mapato nayo yataweza kuongezeka zaidi na hivyo kuwasaidia hata wananchi
wenyewe”aliongeza Lumato.
Awali Kaimu
Mweka hazina wa Halmashauri hiyo ambaye ni bw Munguabella Kakulima
alidai kuwa kwa sasa Halmashauri hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya
kuweza kuongeza vyanzo vya mapato kwani mpaka sasa kuna tofauti kubwa
sana ya ongezeko la mapato katika Halmashauri hiyo ya Arusha Vijijini .
Kakulima
alidai kuwa hapo awali waliaanza na mapato ya Milioni 400 lakini mpaka
sasa wameweza kufikia ukusanyaji wa mapato wa zaidi ya Bilioni 2 jambo
ambalo lengo lake ni kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inaepukana na
tabia ya kuwa tegemezi.
0 comments:
Post a Comment