Wednesday, 22 January 2014

GARI LA GONGA WANAFUNZI WAKIWA KWENYE MCHAKAMCHA NA KUUA WATANO

Picture: Wanafunzi 5 wapoteza maisha Mustapha Sabodo Sekondari kwa kugongwa na gari kwenye mchakamchakaGARI dogo lililokuwa ikitokea eneo la Msijute nje kidogo ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, limepurura wanafunzi waliokuwa kwenye mchakamchaka na kuua wanne papo hapo na mmoja kufia hospitalini.

Aidha wanafunzi wengine 47 walijeruhiwa
.

Wanafunzi hao ni wa Shule ya Sekondari
Mustapha Sabodo.

Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio, hospitalini na kwa kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Steven, zinasema  wakati wanafunzi wa shule hiyo walipokuwa wanakimbia mchakamchaka kando ya barabara ya Mtwara - Lindi, gari dogo lenye usajili wa namba za T 174 AED, liliokuwa likiendeshwa na Baraka Mgwegwe miaka (50), lilipoteza mwelekeo na kuwagonga wanafunzi hao.

Alisema kuwa dereva huyo alijisalimisha mikononi mwa polisi baada ya tukio hilo, na jeshi la polisi linaenelea na uchunguzi zaidi kabla ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Naye Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Saidi Mnyachi, alithibitisha kupokea kwa majeruhi 47, ambapo 26 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa na 21, wakiwemo wasichana 15 na wavulana sita, ambapo wamelazwa wakiendelea na matibabu .

Mnyachi, alisema waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya asubuhi  ni Hailati Saidi, Mwanahamis Mohamed, Nasma Salum na Idda Nguli, ambao miili yao imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

---
Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Lukwangule ya Beda Msimbe.



 

Related Posts:

0 comments: