Friday, 13 September 2013

MWALIMU ACHAPWA VIBOKO 30 NA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAFUNZI MKOANI NJOMBE

Mahakama ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu wa shule ya msingi Ingwachanya. Mwalimu huyo Bw. Romanus Msango mkazi wa  Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) na kumuumiza vibaya sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Bw. Fredrick Lukusa, alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka amabao haukua na shaka yoyote.

Alisema mshakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(!) na 31(!) cha kanuni ya adhabu ya 
mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine. “Natoa adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii kwani vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza,” alisema.

Awali ilidaiwa na mwendesha mashtaka, Edson Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali. Alisema kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo limemsababishia maumivu makali.

“Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvu kazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidhalililsha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundishokwa walimu wengine,” alisema.

Bw. Kusekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda  kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.

Wakati huo huo, watu wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali.

Nickson Mahundi, 
MAJIRA, Ludewa

 

0 comments: