Jiweke katika nafasi ya mzazi, fikiria una watoto wawili wadogo ambao hawajatimu miaka kumi.
Unaamka kuwatizama watoto, huwaoni. Unatizama kote kote, unagundua na gari nalo halipo.
Ni rahisi sana kufikiri kuwa watoto hao wametekwa na mtu aliyetumia gari lako. Kwa hiyo jambo la haraka ni kupiga simu polisi ili kupata usaidizi.
Lakini fikiria mshangao utakaokuwa nao baada ya kutambua kuwa watoto wako wenyewe ndiyo walioamua kujiendesha barabarani.
Hicho ndicho kilichotokea jijini Phoenix, Arizona siku ya Jumatano ya wiki jana.
Akiwaeleza askari polisi kwa uchungu, mama wa watoto wawili, mmoja wa kiume wa umri wa miaka 8 na mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 6, anasema alishituka sana alipofahamishwa kuwa mwanaye

wa kiume ndiye aliyekuwa akiliendesha gari barabarani wakati binti yake akiwa ameketi kwenye kiti cha abiria.
Kutokana na kutokuwa na mafunzo yoyote ya udereva, mtoto huyo aliendesha gari hilo hovyo barabarani, jambo lililosababaisha madereva wengine wa magari wapige simu 911 kuwaeleza kinachoendelea. Kwa bahati, jirani wa watoto hao aliwaona walipolichukua gari na kuingia barabarani, hivyo akaamua kuwafua huku akizungumza na 911 kuwaeleza hatua kwa hatua kuhusu kinachotokea.
Baada ya mama mzazi kupiga simu kuripoti, askari polisi walifuatilia gari hilo wakidhani kweli limetekwa, lakini baada ya ajali waling’amua kuwa watoto hao hawakuwa wametekwa, bali mkubwa ndiye aliyekuwa akiliendesha.

Gari hilo
liligonga mlingoti barabrani na kupata ajali iliyomsababishia majeraha
makubwa binti ambaye hakuwa amejifunga mkanda na kwa bahati mbaya airbag
ya upande alikokaa haikufunguka wakati wa ajali ili kumlinda. Kaka yake
yeye alivunjika kiwiko cha mguu, alikuwa amefunga mkanda na airbag ya
upande wake ilifunguka na kumkinga.
Bado haijafahamika sababu ya watoto hao kuamua kuendesha gari hilo wenyewe na taarifa za awali za polisi zimesema hawana sababu ya kumfungulia mtu yeyote mashitaka kutokana na kisa hicho.
Polisi wamewaasa wazazi kuwa waangalifu na makini kuhakikisha kuwa wamezificha vyema funguo za magari yao ili kuepusha urahisi wa watoto kuzichukua na kuamua kuendesha gari bila ujuzi wowote.

0 comments:
Post a Comment