Tuesday, 3 September 2013

HIZI NDIZO TUHUMA NA KASHFA ZA UFISADI WA MALI ASILI

Imeandikwa na Danson Kaijage, Dodoma, Tanzania Daima — 
WAKATI mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, akimtuhumu Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kuibeba kampuni ya uwindaji ya Leopard Tours Ltd, mwenyewe amejibu mapigo akidai mbunge huyo hajafanya utafiti.

Msigwa aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa Kagasheki alitumia nafasi yake kuiarifu kampuni hiyo kuipatia ekari tano kwa gharama ya dola za Kimarekani 30,000 nusu ya gharama za kawaida dola 60,000 kwa ekari kumi.

Mbunge huyo ambaye pia ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa wizara hiyo, alisema kuwa Kagasheki anaendesha wizara kwa kukiuka sheria na taratibu akitumia mamlaka vibaya.

Msigwa alisema kuwa Kagasheki tangu alipoingia madarakani na kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), sasa hifadhi inaendeshwa bila bodi jambo ambalo ni kinyume.

Alidai kuwa waziri huyo alifanya maamuzi
hayo ya kuibeba kampuni hiyo ya uwindaji bila kuzingatia sheria na kanuni za ugawaji wa vitalu na kwamba alivunja sheria kwa kufanya uamuzi wa moja kwa moja na Leopard Tours wa kushusha viwango vilivyowekwa kisheria bila kutoa tangazo la serikali.

Source: kwa habari zaidi bonyeza hapa www.wavuti.com

0 comments: