Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, ameapishwa kama rais wa nchi hiyo mjini Bamako.
Sherehe kubwa zaidi ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amealikwa zitafanyika baadaye mwezi huu.Wanajeshi wa Ufaransa walisaidia jeshi la Mali kupambana na wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwaka huu.
Mtangulizi wa Keita ambaye kwa sasa ni kaimu rais,
Dioncounda Traore, alisema mnamo Jumatatu kuwa tayari amekabiliana na changamoto kubwa sana ikiwemo kuandaa uchaguzi wa amani na kuweza kudhibiti maeneo yaliyokuwa yametekwa na waasi.
Duru zinasema kuwa bwana Keita atastahili kukabiliana na maswala muhimu zaidi kama vile kuleta uthabiti katika eneo la Kaskazini na kuleta mageuzi katika jeshi pamoja na kupambana na ufisadi.
0 comments:
Post a Comment