Kamati ya Utendaji
ya klabu ya Yanga, itakutana leo jioni katika kikao cha dharura kilichoitishwa
kujadili suala la katibu mkuu mpya raia wa Kenya aliyetimuliwa na wazee wa
klabu hiyo.
Kikao hicho
kimeitishwa ikiwa ni siku moja tu baada ya wazee kumtimua Patrick Naggi raia wa
Kenya ambaye alikwenda klabuni hapo na kujitambulisha ndiye katibu mpya.
Imeelezwa
kamati hiyo itajadili masuala mengine kadhaa, lakini agenda namba moja na kubwa
ni hiyo inayomhusu Naggi.
Naggi
aliyewahi kuwa mkugenzi wa ufundi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) alipewa
saa 24 awe ameondoka na kutogusa tena katika klabu hiyo.
Taarifa
zimekuwa zikieleza kwamba aliletwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf manji lakini
bado hakuna utuhibitisho na taraifa zilieleza Manji alikuwa nje ya nchi katika
kazi zake za kibiashara.
Mkenya
alituhumiwa na wazee hao kwamba hakueleza aliyempeleka klabuni hapo, badala
yake akajitambulisha kwamba anachukua nafasi ya Lawrence Mwalusako.
0 comments:
Post a Comment