Tuesday, 3 September 2013

HABARI ZA HIVI PUNDE UHAMISHO WA FABIO COENTRAO KWENDA MAN U WASHINDIKANA

BAADA YA MADRID KUKATAA KUMTOA KWA MKOPO DAKIKA YA MWISHO

Manchester United imeshindwa kumnasa beki wa kushoto wa Real Madrid Fabio Coentrao, imethibitishwa.
 

Manager David Moyes alijaribu kumpata beki huyo mwenye miaka 25 baada ya kushindwa kumnyakua beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines.
Mpaka leo asubuhi klabu hiyo ya jijini Manchester ilishindwa kuthibitisha kwamba wameweza kufanikisha dili la usajili wa Coentrao.

Lakini jioni hii imethibitishwa kwamba usajili huo haukukamilika.


Kwa maana hiyo ni  Marouane Fellaini pekee kutoka Everton kwa ada ya uhamisho wa £27.5m, ambaye ameongezwa kwenye kikosi cha cha Moyes katika dirisha hili la usajili lilofungwa jana.


Inaaminika kila kitu kilifanyika kabla ya muda wa dirisha la usajili kufungwa - hivyo kukawa kuna saa moja ya ziada kwa klabu hizo mbili kukamilisha taratibu nyingine vizuri.


Lakini Madrid wakasitisha dili hilo wakati jaribio lao la kumsajili beki wa kushoto Guilherme Siqueira kutoka Granada, kushindikana baada ya mchezaji huyo kuamua kujiunga na Benfica.

0 comments: