TORRINGTON (KULIA) AKIFURAHI MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA KUONYESHA MOJA KWA MOJA MECHI ZA LIGI KUU, KULIA KWAKE NI MAKAMU WA RAIS WA TFF, ATHUMAN NYAMLANI, NAYE 'AKIANGUKA' |
Uongozi wa
runinga ya Azam Tv umesema unatarajia kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia
Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini ukakataa kuelezea kwa undani zaidi.
Akijibu
maswali ya waandishi hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv, Rhys
Torrington alisema matarajio yao ni kuingiza mamilioni ya fedha, lakini
hawawezi kuweka hadharani mipango yao ya biashara.
“Kweli
tunatarajia kuingiza mamilioni ya fedha kupitia ligi kuu, hii ni sehemu ya
mikakati ya kutengeneza fedha lakini hatuwezi kuanika mipango yetu.
Hata hivyo,
Torrington aliwataka Watanzania kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni chombo
kinachimilikiwa na Mtanzania.
“Ushauri
wangu ni kwenu kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni ya Mtanzania na sasa itaonyesha
mechi za ligi kuu.
Tutaanza majaribio hivi karibuni na siwezi kuruhusu
matangazo yaende hewani bila ya kuwa na kiwango bora ninachotaka,” alisema.
Azam Tv
inatarajia kuanza majaribio yake wiki hii na kama bosi huyo atakuwa ameridhika
na kiwango itaanza kurusha matangazo yake.
Azam Tv
imeingia mkataba miaka mitatu wa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na
bodi ya ligi ambao thamani yake ni Sh bilioni 5.6 na kila klabu itakuwa ikipata
Sh milioni 100 kila msimu.
CHANZO Salehjembeblog
0 comments:
Post a Comment