Monday, 2 September 2013

UGOMVI WA MKE NA MUME WASABABISHA KIFO CHA MTOTO

Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Aines Zacharia mwenye umri wa miezi mine mkazi wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba mkoani Mbeya, amefariki dunia Septemba Mosi majira ya saa saba mchana alipokuwa akiendelea kupata matibabu katika kituo cha afya Kamsamba kutokana na jeraha alilolipata kichwani baada ya kupamizwa ukutani.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki alisema awali kulikuwa na ugomvi kati ya mama wa mtoto huyo aliyemtaja kwa jina la Priscar Willson aliyekuwa amembeba mgongoni na mumewe Steven Cletus. Alisema ugomvi huo ukiendelea, Cletus alimsukuma mwanamke huyo na ndipo wakajikuta wanamgongesha mtoto ukutani na kumsababishia jeraha kubwa kichwani.

Mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana baada ya tukio hilo na Polisi wanaendelea kumtafuta.

0 comments: