Wednesday, 4 September 2013

BONDIO ALIYEPIGWA NA CHEKA NI KINYOZI KWAO MAREKANI

 


Bondia Phil Williams aliyedundwa na Francis Cheka katika kuwania ubingwa wa dunia uzito wa Super Middle unaotambuliwa na WBF ni kinyozi kwao Marekani.

Williams alipigwa na Cheka baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi Mtanzania huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa wa tatu kuchukua ubingwa wa dunia baada ya Rashid Matumla na marehemu Shaaban Magoma.


Mitandao mbalimbali inaonyesha Williams aliyezaliwa Julai 12, 1977 katika Kitongoji cha Queens, New York nchini Marekani, amekuwa akifanya kazi kama kinyozi katika mji wa Minneapolis ambako anaishi kwa sasa.

Pambano kati ya Cheka na bondia huyo lilikuwa na mvuto zaidi kwa kuwa wawili hao kazi zao za nje si za ofisini kwa kuwa hata Cheka huuza chupa za plastiki zilizotumika katika Mji wa Morogoro.

Kabla ya kupigwa na Cheka kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Williams maarufu kama The Drill, alikuwa amepoteza pambano lake la mwisho kwa kushindwa na bondia kutoka Poland, Andrzej Fonfara katika raundi ya tatu.

Mmarekani huyo alionyesha ushindani mkali kwa Cheka ambaye amekuwa bondia Mtanzania asiyeshindwa katika kipindi hiki, hasa nyumbani.

Taarifa nyingine zimeeleza, Williams alikuwa akisotea malipo yake kutoka kwa promota aliyeandaa pambano ambaye pia alikuwa akilia ‘kupigwa’ kutokana na rundo la tiketi feki.
 
chanzo saleheblog

0 comments: