Imeandikwa
na Mwandishi Maalum — Kufuatia kurejea tena kwa mapigano makali
yaliyotokea wiki iliyopita kati ya majeshi ya Serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (FARD) yakisaidiwa na Jeshi la MONUSCO na kundi
la waasi la M23. Umoja wa Mataifa sasa unajaribu kutafuta suluhu ya
kidiplomasia inayolenga katika kujaribu kuweka sawa hali ya mambo.
Mapingano hayo ambayo siyo tu yanasadikiwa kuliondoa kundi la M23 katika ngome yake ya vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu yamelaaniwa vikali na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu Ban ki Moon hasa baada ya kundi hilo la M23 kusababisha kifo cha mwanajeshi Mtanzania na kujeruhi wengine kumi wakiwamo wanajeshi kutoka Afrika ya Kusini.
Mchakato huo wa kisiasa unafanywa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kanda ya Maziwa Makuu, Bi. Mary Robinson, ambaye amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya jumapili na kutoa rambirambi zake kwa wahanga wa mapigano hayo.

Source: kwa habari zaidi www.wavuti.com
0 comments:
Post a Comment