Wengi wa wachimba migodi wa
dhahabu ambao wamekuwa wakigoma tangu Jumanne nchini Afrika Kusini
wamerejea kazini baada ya waajiri wao kukubali kuwapa nyongeza ya
mishahara.
Kwa mujibu wa maafisa wa chama cha kitaifa cha
wafanyakazi, kampuni nne kati ya saba zimekubali kuwapa nyongeza
wafanyakazi hao ambayo inaaminika kuwa asilimia 8.Wachimba migodi walikuwa wametishia kuwa mgomo wa muda mrefu ungesababisha migodi kufungwa na maelfu ya watu kupoteza kazi zao, kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.
Wanasema kuwa bei ya kuzalisha madini hayo imepanda kwani wamelazimika kuchimba mita nyingi chini ya ardhi kupata madini hayo.
Kwa miaka mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote duniani uikiwa ni asilimia 68 mapema miaka ya sabini lakini mambo yamebedilika sasa ikiwa inazalisha tu asilimia sita ya dhahabu yote duniani, hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP
Chama cha wafanyakazi NUM kinawakilisha takriban asilimia 64 ya wachimbaji wa dhahabu kote nchini humo.
Mwaka jana wananchi wengi waliachwa vinywa wazi wakati polisi walipowaua wafanyakazi 34 wa migodi ya platinum wakati wa mgomo haramu ulioitishwa na chama hasimu cha wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment