Friday, 13 September 2013

KUKU AIFIKISHA HALIMASHAURI MAHAKAMAIN

Picture
HALMASHAURI ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, imeshinda
 kesi iliyofunguliwa na mkazi wa Kijiji cha Nyamakobiti, wilayani humo, Bw. Charari Chacha, akipinga halmashauri hiyo kuuza kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000 baada ya kukataa kulipa mchango wa ujenzi wa Shule ya Msingi Nyamakobiti
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Goody Pamba, alisema kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2000 na hukumu kutolewa katika Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza.

Alisema Bw. Chacha alifungua kesi hiyo namba 46.2008 baada ya kushindwa katika kesi ya awali namba 18/2000 aliyoifungua katika Mahakama ya Mkoa. Aliongeza kuwa, Mahakama ya Rufaa jijini 

Mwanza, ilitoa hukumu Septemba 3 mwaka huu, ambapo Bw. Chacha, alishindwa tena kwa mara ya pili.

Bi. Pamba alisema, hadi sasa gharama zilizotumika kuendesha kesi hiyo tangu mwaka 2000 hazijafahamika. Diwani wa kata hiyo, Bw. Rashidi Mugare, alisema kuanzia mwaka 2000-2013, maendeleo y a kijiji hicho yalirudi nyuma kutokana na wananchi kutochangia shughuli za maendeleo.

“Kila mtu alipotakiwa kuchangia shughuli za maendeleo, alitishia kwenda mahakamani kama alivyofanya Bw. Chacha, wachache ndiyo waliokubali kuchangia. Baadaye Bw. Chacha alimkomboa kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000, hadi sasa kijiji chetu ni cha mwisho katika suala zima la maendeleo kulingana na sumu iliyomwagwa, kimsingi kesi hii ilikwamisha mambo mengi ya maendeleo,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho, kuchangia maendeleo ya elimu ambayo ndio dira ya maisha badala ya kuendeleza malumbano na kufungua kesi mahakamani.Aliwataka wasijiingize kwenye gharama wasizoweza kuzimudu kwa kufungua kesi ambazo hazina tija yoyote kwani suala la maendeleo ni kwa faida ya wananchi, Taifa kwa ujumla. 

Veronica Modest, 
MAJIRA, Serengeti

 

0 comments: