Tuesday, 3 September 2013

KATIBU MKUU WA YANGA LAWRENCE MWALUSAKO AACHIA NGAZI YANGA,



Katibu Mkuu Yanga, Lawrence Mwalusako ameamua kuachia ngazi baada ya kukaimu kwa mwaka mmoja.

Mwalusako amesema amefanya hivyo kwa kuwa makubaliano yao yalilikuwa ni kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.

“Haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu na sasa muda mwafaka umefika wa kufanya hivyo,” alisema hivi punde.


Lakini uchunguzi wa Blog hii umeonyesha kuwa Yanga imeleta Mkenya kuchukua nafasi yake hiyo na tayari ameanza kazi.
Mkenya huyo anajulikana kwa jina Patrick Naggi kuchukua nafasi hyo.
Taarifa hizo zinaaleza Naggi amewahi kuwa Technical Director wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) na CEO wa Tusker ya  Kenya.
 
Chanzo salehejembe blog

0 comments: